Mwakilishi wa mawakibu Husseiniyya katika mji wa Diwaniyya: Idadi ya mawakibu za kutoa huduma imezidi (2000)…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu kimetangaza kua: Idadi ya mawakibu za kutoa huduma ndani ya eneo la mkoa wa Diwaniyya zilizo hudumia mazuwaru wa Arubaini mwaka huu imefika (2214) zilizo sajiliwa rasmi, bila kuhesabu mamia ya Husseiniyya na nyumba za watu pamoja na mawakibu zingine zilizo toa huduma bila kusajiliwa, tena zilianza kutoa huduma tangu siku ya kwanza”.

Akaongeza kua: “Kuna mawakibu zimeenda weka kambi katika mikoa mingine inayo pitiwa na mazuwaru baada ya kumaliza kutoa huduma katika mkoa wao, sambamba na kushiriki katika mawakibu zinazo toa huduma katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zinazo elekea katika mkoa huo”.

Akabainisha kua: “Hakika mawakibu za kutoa huduma, kazi yao haiishii kuhudumia mazuwaru peke yake, bali wanatoa ushirikiano mkubwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama, baada ya kumaliza matembezi ya mazuwaru katika mkoa huu watumishi wa mawakibu hizi wataanza kutembea kuelekea Karbala ili wapate utukufu mara mbili, utukufu wa kutoa huduma na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: