Kuwasili kwao katika malalo mawili matukufu: mawakibu za kuomboleza (matam) zaonyesha picha mpya katika muonekano wa maombolezo ya Arubaini…

Maoni katika picha
Mawakibu za kuomboleza zinaendelea kuwasili katika malalo mawili matukufu ya Sayyid Shuhadaa na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Hujjat bun Hassan (a.f) katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), baada ya kumaliza ratiba ya mawakibu za zanjiil iliyo chukua siku mbili, asubuhi ya leo Juma Pili (18 Safar 1440h) sawa na (28 Oktoba 2018m) zimeanza kuwasili maukibu za matam katika haram mbili tukufu wakiwa wamejaa simanzi na huzuni kubwa.

Matembezi ya maukibu hizi –kama kawaida- yanaanzia katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) na wanaenda kuingia katika uwanja wa haram yake tukufu, na hapo wanalia na kupiga matam wakiwa na huzuni kubwa ya msiba huu, baada ya hapo wanaelekea katika kaburi la mnyweshaji wa maji Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakati wa matembezi yao walionyesha picha ya mwenye kuwahami mateka wa Ahlulbait Imamu Zainul-Aabidina alipo kua anaimba wakati wa kufika katika kaburi la baba yake Hussein (a.s), hadi wanapo ingia katika uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi baba wa uaminifu na kujitolea, hapo wakalia sana baada ya kukumbuka kukatwa mikono miwili ya mnyweshaji wenye kiu Karbala.

Maukibu hizi kutoka ndani na nje ya Iraq zitaendelea kuingia katika Ataba mbili tukufu kwa muda wa siku mbili, chini ya usimamizi na uratibu wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya ambacho kipo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kilicho fuatilia mambo ya kiofisi na kiusalama, sambamba na kuandaa jeduali maalimu linalo onyesha uingiaji wa maukibu hizi na muda utakaotumiwa na kila maukibu, pamoja na kusambaza watumishi wake wanao simamia matembezi kuanzia mwanzo hadi mwisho, kwa namna ambayo haizuwii harakati za mazuwaru wengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: