Katika njia ya Imamu Hussein (a.s) mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda hatuko nao kimiili lakini tupo nao kiroho…

Maoni katika picha
Nyoyo zinanyongea tunapo wakumbuka mashujaa wetu waliopata shahada, na tunapo kumbuka namna walivyo lishinda genge la magaidi lililo taka kuteka ardhi yetu na maeneo yetu matukufu, walijitokeza kwa wingi wakiwa na shauku isiyo elezeka, kabla ya miaka kadhaa walikua wanasimama hapa na kumkaribisha kila anaye tembea kwenda katika ziara ya Arubaini, jana wamesimama na kujitolea kufa kwa ajili ya kuendeleza jambo hili na kumuiga Imamu Hussein (a.s), leo hatupo pamoja nao kimiili lakini tupo pamoja nao kiroho, roho zao zinawakaribisha mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hatuna budi wapenzi wa Imamu na watumishi wake ispokua kuandaa maukibu ya kuomboleza kwa ajili ya kuwakumbuka kwenye njia ya mazuwaru ya (Najafu – Karbala) na kuhusisha vitu vifuatavyo:

  • 1- Kuwaita mazuwaru waingie ndani ya hema la maukibu na kusoma Qur’ani ukurasa mmoja au zaidi na kuzielekeza thawabu za kisomo hicho kwa mashahidi, mwaka jana maukibu hii ilifanikiwa kusoma mamia ya khitima kwa ajili ya mashahidi wa Iraq na Hashdi Sha’abi.
  • 2- Kuendesha visomo vya Qur’ani ndani ya hema au nje kwa kushirikiana na taasisi au jumuiya za Qur’an.
  • 3- Kuonyesha filamu za baadhi ya matukio ya kishujaa yaliyo fanywa na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na namna walivyo weza kukomboa miji iliyokua imetekwa na magaidi wa Daesh.
  • 4- Kugawa machapisho yenye aya za Qur’ani kwa mazuwaru.
  • 5- Hema hizi hazijaishia upande wa wanaume peke yake, bali kuna hema za wanawake pia. Jambo hili linafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo, wanafanya usomaji wa surat Fat-ha na sura fupi fupi pamoja na nyeradi za swala chini ya walimu mahiri wenye uzowefu mkubwa, pia kuna darsa maalumu la watoto.

Kadri muda unavyo kuwa mrefu ndio tunavyo zidi kuwakumbuka na kuwatia rohoni, Mwenyezi Mungu azipe subira familia zenu na akujalieni kuwa waombezi wao siku ya kiyama na akufufueni pamoja na Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: