Mtambo wa kamera za ulinzi uliofungwa na Atabatu Abbasiyya tukufu miaka miwili iliyo pita ni miongoni mwa mitambo ya kisasa na wenye ubora mkubwa hapa Iraq, mtambo huu unasifa nyingi zinazo ufanya uwe na umuhimu mkubwa katika idara ya mawasiliano, unauwezo wa kufanya kazi mfululizo na kwa kiwango kikubwa, kazi yake kubwa ni kuimarisha usalama na kuweka utulivu kwa mazuwaru kwa kumbani mtu yeyote atakaye taka kufanya jambo la uvunjifu wa amani, umekua msaada mkubwa wa kitengo cha nidhamu katika kuimarisha usalama hasa kwenye ziara ya Arubaini.
Muhandisi Farasi Abbasi Hamza ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kamera za mtambo huo kwa sasa zinaangalia eneo linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuangalia usalama na sehemu zenye msongamano mkubwa wa mazuwaru, hali kadhalika tunatumia kamera hizo kuangalia katika barabara zilizo karibu na Ataba kama vile barabara ya Jamhuriyya, barabara ya Baabu Bagdad pamoja na barabara za mbali, kama vile barabara ya Maitham Tammaar pamoja na kuangalia ndani ya haram, zinatusaidia kuangalia jambo lolote baya pamoja na wizi kama ukitoteo, pia kamera hizo zinaonyesha vituo vya ukaguzi na sehemu za kuingia na kutoka mazuwaru (milangoni)”.
Akaongeza kua: “Kuhusu uangaliaji wa harakati za mawakibu kuna kamera maalumu, ambazo zinaangalia kila kinacho fanywa na mawakibu wanapo kua katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na wanapo ingia na kutoka katika Ataba mbili tukufu, kwa ajili ya kuhakikisha hakuna tatizo linalo tokea pamoja na kuwaangalia waokowaji na kuwalekeza sehemu wanayo hitajika”.