Kitengo cha maadhimisho na mawakibu: Jumla ya maukibu (227) za kutoa huduma na kuomboleza kutoka katika nchi (23) zimekuja kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) mwaka huu…

Maoni katika picha
Kiengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetangaza idadi ya mawakibu za kutoa huduma zilizo shiriki mwaka huu katika kuhuisha ziara ya Arubaini katika mji wa Karbala, rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Idadi ya mawakibu zilizo shiriki mwaka huu kutoka nchi za kiarabu na zisizo kua za kiarabu zimefika (227) kutoka katika nchi (23) ambazo ni: (Omani, Baharain, Kuwait, Saudia, Yemen, Lebanon) nchi za kiarabu, na zisizo kua za kiarabu ni (Adharbaijaani, Iran, Afghanistani, Swiden, India, Marekani, Indonesia, Pakistani, Ubelgiji, Tailendi, Uturuki, Tanzania, Uingereza, Kanada, Holandi, Ufaransa, Kenya).

Akaongeza kusema kua: “Hakika kitengo kiliandaa vibali rasmi vya kukaa maukibu hizo kwa ajili ya kushiriki katika maombolezo haya, na kuwawekea wepesi katika maswala ya kiusalama na kiidara”. akabainisha kua: “Maukibu hizi hazikuwepo katika mji wa Karbala peke yake bali zilikuwepo pia katika njia zinazo elekea Karbala”.

Salmaan akasema: “Maukibu hizo hazikuishia kugawa chakula na vinywaji tu bali kuna ambazo zilishiriki katika matukio ya uombolezaji pia (matam na zanjiil)”.

Tunapenda kusema kua mji mtukufu wa Karbala unashuhudia ongezeko la maukibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyo kuja kuhuisha kumbukumbu ya ziara ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s) na kuhudumia mazuwaru wake kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: