Bado tupo katika mwezi wa Safar, zimepita siku nne tangu kumalizika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), bado mazuwaru wengi wapo katika mji wa Karbala hadi wakati huu wa kuandikwa habari hii, mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ahmadi Swafi alizungumzia tatizo la usafiri kua: “Napenda kusema tatizo linalo jirudia kila mwaka, inatakiwa wahusika watafakari kwa kina namna ya kutatua tatizo hili, tatizo la usafiri, katika kila ziara tunasema jambo hili, tatizo barabara zinazo ingia na kutoka katika mji wa Karbala haziendani na idadi kubwa ya mazuwaru wanaokuja”.
Aliyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa (23 Safar 1440h) sawa na (2 Novemba 2018m), katika uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s), akaongeza kua: “Sidhani kama jambo hili haliwezi kutatuliwa, bali linahitaji kutafakari kwa kina, na kuweka mkakati wa kufungua milango (barabara) za kuingua na kutoka kwa urahisi katika mji huu, jambo hilo ndio litakalo ondoa usumbufu kwa mazuwaru, hatuna tatizo la mabasi au gari za kubeba watu, tatizo letu ni barabara, sidhani kama kuna mji unaoshinda mji huu duniani (kwa kuingiza watu wengi) kila mwaka tunarudia ombi hili lakini hakuna anaye tusikiliza wala hakuna juhudi zozote za kutatua tatizo hili”.
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza rasmi idadi ya mazuwaru walio sajiliwa na mtambo wa kuhesabu watu wa kielektronik uliofungwa katika barabara kuu tano, ambazo ni: (Bagdad – Karbala, Baabil – Karbala, Najafu – Karbala, Husseiniyya – Karbala, Huru – Karbala) ya kua wamefika (15,322,949) mazuwaru hao walianza kuhesabiwa mwezi (7 Safar) hadi mwezi (20 Safar) 1440h saa sita usiku.
Bado Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia watumishi wao wa vitengo vyote wanaendelea kuwahudumia mazuwaru waliopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili na katika barabara zinazo elekea Ataba mbili tukufu, na kuwarahisishia safari za kurejea katika miji yao.
Tunapenda kukumbusha kua huduma zinazo tolewa na watumishi wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zitaendelea hadi pale atakapo ondoka zaairu wa mwisho katika mji huu, kisha wataendelea kufanya kazi kama walivyo kuwa wakifanya katika siku za kwaida.