Mwendelezo wa ukarimu wa mwenye malalo tukufu: Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaendelea kugawa chakula kwa mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaendelea kugawa chakula kwa watu waliokuja katika ziara ya Arubaini kwenye malalo mawili matukufu, malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kupita siku sita tangu kumalizika kwa ziara ya Arubainiyya ambayo mgahawa huu uligawa zaidi ya sahani za chakula (elfu 75) kwa siku, bado unaendelea kugawa chakula kwa mazuwaru walio fika katika mji wa Karbala hivi karibuni au wanao endelea kubaki katika mji huu na wengi wao wanatoka nje ya Iraq.

Rais wa kitengo cha mgahawa bwana Kaadhim Abada ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi yetu ya kugawa chakula kwa mazuwaru wa Arubaini haiishii baada ya kuisha kwa ziara, huendelea hadi baada ya ziara, jambo hili hutokea katika kila msimu wa ziara, huwa tunaendelea kugawa chakula hadi baada ya kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), na hutegemea wingi wa mazuwaru, kila mazuwaru wanavyo kuwa wengi ndio tunavyo endelea kutoa huduma, kila siku tunagawa maelfu ya sahani za chakula kupitia dirisha la kugawa chakula la nje, na tunagawa mara mbili kila siku”.

Akaongeza kua: “Jambo lililo tusukuma kugawa chakula, ni pale tulipo ona maukibu nyingi za kugawa chakula zimefunga rasmi utowaji wa chakula kwa mazuwaru wa Arubaini, hapo tukaona ulazima wa mgahawa kuendelea kugawa chakula kama ulivyo kua ukigawa siku za kwanza za mwezi huu wa Safar, kwa nini isiwe hivyo wakati ni muendelezo wa ukarimu wa mwenye malalo hii tukufu”.

Kumbuka kua mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulikua unagawa chakula saa (24) kila siku katika kipindi cha ziara ya Arubaini, na ulikua unapokea wageni na kuwaandalia chakula, ulikua unagawa zaidi ya sahani za chakula (elfu 75) kila siku, kwa milo mitatu mikuu, ulikua unagawa chakula kupitia ukumbi wa mgahawa au katika madirisha ya nje yapatayo sita, sambamba na vyakula vyepesi vyepesi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: