Vituo vya kuelekeza walio potea vya Atabatu Abbasiyya tukufu: Mazuwaru (9,869) walio potea katika ziara ya Arubaini tulifanikiwa kwa asilimia kubwa kuwakutanisha na jamaa zao…

Maoni katika picha
Muhandisi Farasi Abbasi Hamza kiongozi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ndio idara iliyo simamia mabanda ya kuelekeza walio potea na kupotelewa amesema kua: “Idadi ya watu walio potea na walio potelewa katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) walio sajiliwa katika mabanda (35) ya kuelekeza walio potea wamefika mazuwaru (9,869) (tulio taarifiwa rasmi na jamaa zao kuhusu kupotea kwao) asilimia kubwa tuliwakutanisha na jamaa zao”.

Akasema kua: “Jambo la kumkutanisha aliye potea na jamaa zake hupewa umuhimu mkubwa sana husasan watoto na wazee, jambo hilo linathawabu nyingi katika upande wa kusaidia wenye shida, hali inakuwaje unapo msaidia zaairu wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), kutokana na wingi wa watu, zaairu anaweza kumpoteza ndugu yake, akajikuta anajishughulisha na kumtafuta huku roho yake ikiwa na wasisi sana na kukosa amani hadi atakapo mpata”.

Akaongeza kua: “Kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), tumeboresha mabanda ya kuelekeza walio potea, ambayo yamekua yakifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka tisa kutokana na umuhimu wake katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, kwa sababu yanagusa hisia za baadhi ya mazuwaru wanaopoteza jamaa zao au ndugu zao katika misongamano ya watu, tulikua wa kwanza kuleta fikra ya kutoa huduma hii kwa mazuwaru na kuingiza utulivu na amani katika nyoyo zao wakati wakiwasubiri jamaa au ndugu walio wapoteza”.

Akabainisha kua: “Mradi huu umepitia hatua tofauti, kwanza tulikua tunagawa simu za bure kwa ajili ya kuwasiliana baina ya mabanda ya (Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, Bagdad – Karbala na Karbala mjini), kisha tukaboresha na kuyafanya mabanda hayo kuweza kupiga simu sehemu mbalimbali ndani ya Ataba, kisha tukaongeza wigo wa mawasiliano hati katika vituo vya mipakani na katika viwanja vya ndege, kwa kushirikiana na Atabatu Alawiyya na baadhi za taasisi na kwa kutumia njia za mawasiliano za kisasa”.

Muhandisi Farasi akabainisha kua: “Tumetengeneza program ya kielektronik na kuisambaza katika mabanda yote kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya tukufu, mradi huu umepata mwitikio mkubwa sana katika miaka sita ya mwisho, jambo lililo pelekea mradi huu tuupe umuhimu mkubwa zaidi mwaka huu, na kuufanya uweze kumpata mtu aliye potea kwa kutumia picha yake ndani ya muda mfupi zaidi, na sasa kwa kutumia intanet tunaweza kumtafuta mtu aliye potea kila sehemu ya dunia sio ndani ya Iraq peke yake, jambo hili limesaidia kwa kiasi kikubwa kuwapata walio potea kwa urahisi”.

Kumbuka jumla ya watu walio potea na kupotelewa katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) walifika (9,869) ambao wamesajiliwa katika mabanda ya kuelekeza walio potea na walio potelewa ambayo yapo (35) katika barabara zinazo elekea katika mji mtukufu wa Karbala, mabanda hayo yanavifaa vya kisasa zaidi vya mawasiliano, yana kombyuta, screen, kamera na vinginevyo, pamoja na kuandaa sehemu za kukaa watu walio potelewa wanao subiri kukutanishwa na jamaa zao kwa muda wa saa (12), sehemu hizo zinasimamiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu walio jitolea kutoka mikoa tofauti ya Iraq, asilimia kubwa ya watu walio potea walikutanishwa na jamaa zao, vituo vya kuongoza walio potea na walio potelewa vimewekwa katika pande nne zifuatazo:

  • a- Upande wa Najafu – Karbala.
  • b- Upande wa Baabil – Karbala.
  • c- Upande wa Bagdad – Karbala.
  • d- Upande wa mjini (katikati ya mji wa Karbala).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: