Kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w): Atabatu Abbasiyya tukufu yaandaa ratiba ya kuomboleza msiba huo…

Maoni katika picha
Katika kukamilisha ratiba ya msiba iliyo andaliwa wakati wa kuomboleza kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalumu ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliye fariki siku kama ya kesho tarehe (28 Safar 1440h), ratiba hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Ataba tukufu katika kuomboleza msiba huu mkubwa sana katika umma wa kiislamu.

Ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • 1- Kitengo cha maadhimisho na mawakibu ambacho kipo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimeandaa utaratibu maalumu wa kuzipokea mawakibu za kuomboleza zinazo kuja kuzuru kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • 2- Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa wazungumzaji watakao toa mawaidha ndani ya uwanja mtukufu wa haram, kuhusu Mtume Muhammad (s.a.w.w), ikiwa ni pamoja na muhadhara rasmi kwa watumishi wa ataba utakao tolewa ndani ya ukumbi wa utawala.
  • 3- Kitengo cha usafirishaji kimeandaa gari (20) kwa ajili ya kubeba maukibu za watu wa Karbala na kuwapeleka Najafu katika kaburi la kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).
  • 4- Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kitatangaza matembezi wa watu wanaokwenda Najafu, sambamba na kuonyesha matukio ya kuomboleza kifo cha Mtume yatakayo fanyika ndani ya uwanja wa haram ya Alawiyya na ndani ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
  • 5- Kutakua na matembezi ya maukibu ya pamoja baina ya Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kutoa pole wa bwana wa Mashahidi abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • 6- Kuchapisha toleo la nakala za jarida ya Alkafeel na Alkhamisi zinakazo elezea tukuo hili chini ya idara ya utafiti, na kuzigawa kwa mazuwaru wa Karbala katika usiku wa Ijumaa.
  • 7- Kuindaa kipindi kinacho elezea tukio hili na umuhimu wa kuomboleza kitakacho rushwa na Idhaatul-Kafeel.

Kumbuka kua waislamu wa Dunia nzima wanaomboleza msiba huu wa kifo cha Mtume wa mwisho na Mbora wa Manabii Muhammad bun Abdullahi (s.a.w.w), aliye kufa mwezi ishirini na nane Safar mwaka (11) hijiriyya, akiwa na umri wa miaka stini na tatu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: