Atabatu Abbasiyya yafanya majlis ya kuomboleza kifo cha Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya Juma Tano ya leo (28 Safar 1440h) sawa na (7 Novemba 2018m) umefanya majlis maalim kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ndani ya ukumbi wa utawala katika haram tukufu ya Abbasi, hii ndio kawaida yake katika kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mzungumzaji katika majlis hiyo alikua ni shekh Haidari Aaridhiy kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, amezungumzia tabia na ubinaadamu wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na mambo mengine matukufu katika historia yake, na kwa namna gani waislamu wanatakiwa kufuata mwenendo wake na kutekeleza mafundisho yake, na kwamba ujumbe wake ndio ujumbe bora kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), kisha akamaliza mawadha yake kwa kusoma kaswida iliyo amsha hisia za huzuni za msiba huu mkubwa katika umma wa kiislamu.

Kumbuka kua leo (28 Safar) ni siku ya kukumbuka kifo cha mbora wa viumbe na mwisho wa Manabii Mtume Muhammad (s.a.w.w), waislamu kote Duniani wanaomboleza msiba huu, na sehemu kubwa ya waombolezaji huelekea katika mji wa Najafu kufanya ziara katika kaburi la kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib ambaye ni mtoto wa Ammi yake Mtume na khalifa wake (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: