Jufunze kiarabu kutoka katika Qur’ani tukufu, chapisho jipya lililo tolewa na kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha…

Maoni katika picha
Kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya kimetoa chapisho jipya kwa jina la: (Jifunze kiarabu kutoka katika Qur’ani tukufu) ambalo ni miongoni mwa machapisho ya (Jifunze kutoka katika Qur’ani tukufu), hiki ni kitabu cha kwanza cha aina hii kutolewa na kituo hiki, kinacho lenga kujifunza lugha ya kiarabu na usomaji sahihi wa kitabu kitakatifu kwa njia mpya na ya kuvutia kwa wale wasio zungumza kiarabu.

Mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidiy amesema kua: “Kujifundisha lugha ya kiarabu ni ufunguo wa kujifunza Qur’ani tukufu na tafsiri yake pamoja na elimu zingine za sheria zinazo hitajiwa na kila muumini”.

Akasisitiza kua: “Asilimia kubwa ya waumini wanaoishi katika nchi zisizo zungumza kiarabu wanahitaji kujifundisha lugha hii, hususan inapo fundishwa kutoka ndani ya Qur’ani, wanapata mambo mawili kwa wakati mmoja, wanajifunza lugha pamoja na usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu”.

Akabainisha kua: “Kitabu hiki kina juzuu moja lenye kurasa (108), kimeandikwa kama kitabu cha kufundishia, ukubwa wa karatasi zake ni (A4) kina aya za Qur’ani zinazo endana na kiwango cha watu wanao anza kujifunza kiarabu, pamoja na kutenganisha vizuri maneno katika aya, pamoja na rekodi za sauti, maana za maneno na namna ya utamkaji wa herufi za kiarabu, alama za irabu na vinginevyo, pia kuna mazowezi mbalimbali kwa ajili ya kupima uwelewa wa mada”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: