Kwa mwitikio mkubwa: Maahadi ya Qur’ani tukufu yahitimisha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru wa Amirul Mu-uminina (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio makubwa yaliyo patikana katika vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwenye msimu wa ziara ya Arubaini, leo hii Maahadi ya Qur’ani kupitia tawi lake la mkoa wa Najafu yahitimisha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru wa Amirul Mu-uminina (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Uongozi wa Maahadi umesema kua vituo vya kufundisha Qur’ani viliwekwa katika barabara zote zinazo elekea kwenye haram tukufu hususan zile zinye msongamano mkubwa wa mazuwaru, kwa ajili ya kuhakikisha tunanufaika na ziara hii tukufu, vituo hivyo vilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru walio jitokeza kwa wingi kujifundisha usomaji sahihi wa Qur’ani hasa sura wanazo soma kila siku katika swala pamoja na adhkaari zake.

Tawi la Maahadi katika mkoa wa Najafu limetumia uwezo wake wote kwa ajili ya kufanikisha awamu ya pili ya mradi huu, baada ya kupewa kila kinacho hitajika na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kufanikisha mradi huu ambao ni kielelezo cha kufuata usia wa Mtume (s.a.w.w), wa kushikamana na Qur’ani pamoja na kizazi chake kitukufu, hii ni fursa nzuri ya kujifundisha usomaji sahihi wa Qur’ani pamoja na adhkaari za swala ambazo ni sharti muhimu la kusihi kwa faradhi hiyo tukufu.

Mazuwaru wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Qur’ani kwa kuendesha mradi huu muhimu, wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu pamoja na adhkaari za swala mambo ambayo ndio sharti kubwa la kusihi kwa faradhi hiyo tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: