Nukta muhimu alizo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa…

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa kwenye uwanja wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) leo (1 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (9 Novemba 2018m) chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, miongoni mwa nukta alizo ongea ni:

  • - Kwa ujumla mwanaadamu anawajibika kufanya kazi katika maisha yake.
  • - Moja ya mambo yaliyo tufikisha hapa ni kukosekana misingi ya uwajibikaji wenye mafanikio.
  • - Kutekeleza wajibu wako wakati mwingine huchukuliwa kama tendo la kibinaadamu.
  • - Kufanya kazi na kutekeleza wajibu ni msingi ambao humsaidia mtu kufikia malengo.
  • - Kutofanya kazi na uvivu ni sababu kubwa ya kufeli.
  • - Kufanya kazi na kuwajibika ni msingi muhimu unao waunganisha watu.
  • - Uislamu umehimiza kufanya kazi, na uchumi ni kitu muhimu kwa mwanaadamu kinacho muwezesha kutekeleza majukumu yake katika maisha.
  • - Uislamu umekemea kuacha kufanya kazi na umetahadharisha uvivu na uzembe na ukabainisha madhara yake.
  • - Kazi zinazo fanywa na mwanaadamu zipo chini ya uangalizi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na waumini.
  • - Uislamu umetahadharisha uvivu na uzembe kazini au katika kutekeleza majukumu.
  • - Uislamu unamuheshimu mwanaadamu kutokana na utendaji wake wa kazi.
  • - Kufanya kazi ni ibada kubwa.
  • - Uislamu unachukulia kufanya kazi inayo kuwezesha kupata matumizi yako na ya familia yako ni sawa na kupigana jihadi, na mtu anaye fanya kazi ni bora zaidi kushinda mtu anayetawa ndani na kufanya ibada bila kufanya kazi.
  • - Miongoni mwa majukumu ya mwanaadamu ni kujenga juu ya ardhi na kuleza maendeleo katika jamii yake.
  • - Tunatakiwa kuhisi kua kufanya kazi ni msingi wa kimaumbile na kibinaadamu.
  • - Hatuwezi kutekeleza majukumu yetu hapa duniani bila kifanya kazi, yatupasa kutambua kua kufanya kazi ni matakwa ya kiungu na kibinadamu.
  • - Ili kupata mafanikio ya mtu mmoja mmoja au jamii ni lazima kufanya kazi,
  • - Kinacho sikitisha jamii ya watu wa Iraq wahatekelezi misingi ya uwajibikaji yenye kuleza mafanikio kazini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: