Kwa picha: Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yavua vazi la huzini za Husseiniyya…

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia mwezi wa Rabiul Awwal na kumalizika msimu wa huzuni za Aali Muhammad (a.s) watumishi wa Atabatu Abbasiyya wameondoa mapambo meusi katika haram tukufu yaliyo wekwa mwanzoni mwa mwezi wa Muharam hadi mwishoni mwa mwezi wa Safar, kuondolewa kwa mapambo meusi ni ishara ya kumalizika msimu wa huzuni za Husseiniyya ambazo zimedumu miezi miwili mfululizo, kipindi chote hicho haram ilikua imejaa waombolezaji waliokuja kutoka kila sehemu ya dunia.

Kazi ya kuondoa mapambo meusi ilianza kwa kushusha pendera nyeusi iliyopo juu ya kubba tukufu na kupandisha bendera nyekundu, kisha wakatoa mapambo meusi yeto yaliyo wekwa katika kaburi tukufu na sehemu zote zinazo zunguka kaburi, kisha yakatolewa mapambo na mabano meusi yaliyo wekwa katika kuta na nguzo za uwanja wa haram tukufu upande wa ndani na nje, milangoni na kwenye korido za haram, kama ishara ya kumalizika msimu wa huzuni uliodumu kwa miezi miwili.

Tunapenda kufahamisha kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu huvishwa vazi jeusi kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo kila mwaka, kipindi hicho huitwa kipindi cha huzuni, ambacho huwa ni kila mwezi wa (Mhuram na Safar), ndani ya kipindi hicho kuna ziara ya Ashura na Arubaini pamoja na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan, Imamu Zainul-Aabidina na kumalizia kwa kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: