Mwezi tano Rabiul Awwal ni siku aliyofariki mtoto wa Imamu Hussein bibi Sakina (a.s)…

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi tano Rabiul Awwal ulitokea msiba katika nyumba ya Mtume (s.a.w.w) mwaka (117h) miaka (56) baada ya tukio la Twafu, ni siku aliyo fariki bibi Sakina (a.s) mtoto kibenzi wa Imamu Hussein (a.s).

Bibi Sakina (a.s) jina lake kamili ni Amina binti Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), mama yake anaitwa: Rubaab binti Amri Alqais bun Adi Alkalbiy, amejulikana zaidi kwa jina la (Sakina) kwa sababu alikua mpole, mtaratibu na mnyenyekevu.

Alizaliwa mwaka wa arubaini na saba hijiriyya, wakati wa kifo cha baba yake Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala alikua na umri wa miaka kumi na nne, ambayo aliishi chini ya usimamizi na malezi matukufu ya baba yake bwana wa mashahidi (a.s), kupata malezi ya maasumu moja kwa moja ndio kulimjenga katika elimu, Dini na tabia, pamoja na kuathirika na mazingira ya familia yenye zaidi ya maasumu mmoja na watukufu wengine, alikua na haki ya kua mtu bora mwenye elimu kubwa na mtakatifu.

Baada ya tukio la Twafu manyanyaso yaliyo endelea aliyashuhudia na alikua mpambanaji katika njia ya baba yake kwa kutumia elimu, nguvu na imani. Baada ya kifo cha baba yake alikua chini ya usimamizi na malezi ya kaka yake Imamu Sajjaad (a.s), maisha yake yalijaa elimu na adabu njema katika jamii, hata wabaya wake walimsifu kwa tabia njema, hakika bibi Sakina alikua mwanamke bora katika zama zake, alikua ni mtambuzi, mwenye akili ya hali ya juu, mwenye adabu na mwenye kujistiri, alizipamba majlisi za watu wa Madina kwa elimu yake, tabia yake na uchamungu wake, alikua mfasaha, baba yake Imamu Hussein (a.s) alishuhudia ibada zake na tahajudi zake, anasema: “Amma Sakina amezama katika kumuabudu Allah”, aliyasema hayo pale Hassan bun Hassan mtoto wa ammi yake (a.s) alipotaka kumposa akamchagulia dada yake Fatuma.

Bibi Sakina (a.s) alifariki tarehe 5 Rabiul Awwal 117h, katika mji wa Madina na akazikwa katika makaburi ya Bakii kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Shadharaatu Dhahabu, na kunakiliwa na Sayyid Muhsin Amiin katika Aayaani yake kua: Alifia katika mji wa Madina baada ya miaka hamsini na tano (ya tukio la Twafu) katika mwezi wa Rabiul Awwal mwaka wa 117h. ni mashuhuri kua alizikwa Madina. Amani iwe juu yake bibi mtukufu mwenye elimu siku aliyo zaliwa na siku aliyo kufa na siku atakayo fufuliwa Inasha Allah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: