Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanasema: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Swahibu Zamaan…

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wametuma rambirambi kwa Imamu wa zama Hujjat Muntadhar (a.f) kutokana na kifo cha baba yake Hassan Askariy (a.s), ambaye kumbukumbu ya kifo chake inasadifu Ijumaa ya kesho, wamefanya matembezi ya kuomboleza baada ya Adhuhuri ya leo Alkhamisi (7 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (15 Novemba 2018m) kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu mkubwa.

Matembezi hayo yanachukuliwa kama mwanzo wa utekelezaji wa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika msiba huu, yalianzia ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili, huku wakiimba kaswida zilizo mtaja Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) na kumpa pole kutokana na kifo cha baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), walipo wasili katika haram ya bwana wa mashahidi (a.s) walipokelewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, waliungana pamoja na kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s), katika majlisi hiyo ziliimbwa kaswida za huzuni na mashairi yaliyo amsha hisia za majonzi katika nyoyo za waumini kufuatia msiba huu mkubwa.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha tangaza msiba na imewekwa mapambo meusi kwa ajili ya msiba huu, pamoja na kuandaa ratiba maalumu ya uombolezaji (Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Swahibu Zamaan kutokana na msiba huu mkubwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: