Dondoo ya kumbukumbu uimizayo: Kifo cha Imamu wa kumi na moja Hassan Askariy (a.s)…

Maoni katika picha
Imamu Askariy (a.s) alikufa kwa sumu, tarehe nane Rabiul Awwal mwaka wa (260h), akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, ilikua siku ya huzuni katika mji wa Samara, baada ya kusambaa taarifa za kifo chake watu walifurika nyumani kwake huku wanalia, wanahistoria wameifananisha siku hiyo na siku ya kiyama, kwa nini? Kwa sababa ya wingi wa watu walio kwenda msibani na wakawa wanazungumza utukufu wake, hadi utawala ukapata mshtuko.

Imamu Hassan Askariy (a.s) alichukua madaraka ya Uimamu rasmi baada ya kifo cha baba yake Imamu Ali Haadi (a.s) mwaka wa (253h), utawala wa Abbasiyya haukumsahau Imamu Hassan Askariy (a.s), walimuweka chini ya uangalizi mkali, walifuatilia harakati zake zote, hadi harakati za utekelezaji wa majukumu yake ya kiuongozi katika umma, hivyo Imamu alikua anatekeleza majukumu yake kwa siri ili bani Abbasi wasimuone, kwa hiyo alipanga watu miongoni mwa wafuasi wake na kuwatumia, ushahidi wa kihistoria unathibitisha kua Imamu alitumia njia ya siri kwa umakini mkubwa.

Imamu Hassan Askariy (a.s) alipata misukosuko kama waliyo pata baba zake watukufu (a.s), aliishi katika mazingira magumu ya kisiasa yaliyo jaa dhulma na ukatili, alipata tabu kulinda misingi ya uislamu mtukufu ambalo ndio jukumu lake alilopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, utekelezaji wa jukumu hilo ulimgharimu sana, alivumilia kukaa jela na manyanyaso mbalimbali.

Imamu aliishi katika zama za mtawala wa kibani Abbasi aitwae Mu’taz, kisha akaja Muhtada, halafu akaja Mu’tamad, watawala wote watatu walimbana sana Imamu na kumnyanyasa, alitekwa mara nyingi, mtawala wa mwisho aliye muua Imamu (a.s) anaitwa Mu’tamad, alikua mtawala anayependa starehe na mambo machafu, alikua anafanya mambo ya haram wazi wazi jambo lililopelekea watu wengi wamchukie, Imamu alinyanyaswa sana na Mu’tamad, aliwekewa ulinzi mkali mno, alichunguzwa na kudadisiwa kila aliyetaka kuwasiliana na Imamu, jambo kubwa lililo sababisha watawala wa bani Abbasi wambane Imamu kiasi hicho ilikua ni husda kwake kutokana na heshima aliyo nayo katika umma, na walikua wanahofia mtoto atakaye mzaa ambaye ni Imamu Mahadi Msubiriwa (Almuntadhar) (a.s), ambaye walikua wanatambua wazi kwamba atazaliwa na Imamu Hassan Askariy (a.s).

Ndio ikapelekea hadi Mu’tamad akampa sumu kali iliyo athiri mwili wa Imamu (a.s) na ikamuuguza siku kadhaa akawa amelala na kuugulia maumivi hadi alipo fariki akiwa na umri wa miaka ishirini na nane, ambapo ulikua mwaka wa (260h), akazikwa pamoja na baba yake Imamu Haadi (a.s) katika nyumba yake huko Samara, sehemu ambayo kaburi zao zipo hadi sasa na zimekua mwelekeo wa waumini na wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), watu huenda kutabaruku na kutawasal kwa mwenyezi Mungu kwa utukufu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: