Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba maalumu ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) msiba huu mkubwa kwa waislamu wote na kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Ijumaa ya leo (8 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (16 Novemba 2018m) wamefanya majlisi maalumu kwa watumishi wake ndani ya ukumbi wa utawala, ni kawaida kufanya hivi kila kwenye tukio la huzuni kwa Ahlulbait (a.s).

Katika majlisi hiyo palikua na muhadhara wa Dini uliotolewa na Sayyid Adnaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa mambo aliyo zungumza ni:

 • - Mtoto wa Imamu Askariy (a.s) Imamu Mahadi (a.f) atafanikisha ndoto ya Mitume (a.s) kwa kueneza uadilifu na amani Dunia nzima, baada ya kujaa dhulma na uovu.
 • - Mambo tunayo shuhudia leo Duniani yanatokana na kuipindua serikali ya Mwenyezi Mungu kwa kuwakataa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuwanyima haki ya kuunda serikali adilifu.
 • - Hekima ya kiongozi wa waumini (a.s) na subira yake aliweza kulinda misingi ya Dini tukufu ya kiislamu, na alikirithisha kizazi chake.
 • - Mwenyezi Mungu mtukufu ameilinda Qur’ani kupitia Mtume Muhammad na watu wanyumbani kwake watakasifu (a.s).
 • - Maadui wa uislamu walijaribu kupotosha watu na kuitenganisha Qur’ani na Ahlulbait (a.s).
 • - Kuna hadithi nyingi zinanasibishwa na Mtume (s.a.w.w) lakini hazina ukweli wowote.
 • - Kuwanyanyasa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuwauwa ilikua moja ya njia za kuonyesha chuki kwao.
 • - Imamu Askariy (a.s) alivumilia manyanyaso mengi kutoka kwa watawala wa Abbasiyya.
 • - Imamu Askariy (a.s) aliishi katika zama za watawala watatu waovu wa bani Abbasi, kuanzia Mu’taz hadi Mu’tamad baada ya Muhtada, wote walimnyanyasa na kumuwekea ulinzi mkali.
 • - Sababu kubwa ya kunyanyasa na kuwekwa chini ya uangalizi mkali ni kwakua walikua wanajua atamzaa Imamu Mahadi (a.f).
 • - Imamu Askariy (a.s) alikua anahamishwa jela moja hadi nyingine kila wakati.
 • - Muujiza wa simba, ambao umebakia katika historia ya Imamu Askariy (a.s), ni dalili ya wazi inayo onyesha Uimamu wake.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza msiba huu, na imewekwa mapambo meusi kama ishara ya msiba, pia Alasiri ya jana Ataba mbili tukufu zilifanya matembezi ya kuomboleza msiba huu na kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: