Katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sauti murua za usomaji wa Qur’ani tukufu zasikika…

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani tukufu chini ya Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya katika mradi wake wa Qur’ani uitwao (Arshu-Tilaawah), kimezowea kufanya kikao cha usomaji wa Qur’ani kila siku ya Ijumaa, na hushiriki jopo la wasomi wa Qur’ani tukufu, baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na ziara ambazo hufanyika mwezi wa Muharam na Safar, leo wamerudi kuendesha kikao cha Arshu-Tilaawah katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa sauti murua kabisa, usomoji huu unasadifu sherehe za maulidi ya Mtume pamoja na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Jafari (a.s).

Kikao hiki kimehudhuriwa na msomaji wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Haani Mussawiy, na msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Faisal Matwar na Muhammad Ali Rashidi mmoja wa wanafunzi wa Darul Qur’ani ya Atabatu Alawiyya tukufu na wanafunzi wa mradi wa kiongozi ambao upo chini ya tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, na Baaqir Bayani kutoka shule ya Qur’ani katika wilaya ya Khadhar, na mmoja wa wanafunzi kutoka katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, wamesoma Qur’ani kwa sauti murua zilizo burudisha masikio ya wahudhuriaji, vilevile kulikua na ushiriki mzuri wa usomaji wa mashairi ambayo yaliamsha hisia za furaha kwa wahudhuriaji na mashairi hayo yalisomwa na Abu Hussein Rabii.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya miradi ya Qur’ani tukufu inayo husisha watu wengi, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu-Tilaawah, nao ni mradi unaolenga kunufaika na vipaji walivyo navyo vijana wa Iraq katika usomaji wa Qur’ani, na kuvidhihirisha vipaji vyao katika ulimwengu wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: