Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Landan lafanya mashindano ya Qur’an kwa mara ya kwanza nchini Uingereza…

Maoni katika picha
Katika mnasaba wa kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w), maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Landan ambalo lipo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, limefanya mashindano ya kusoma Qur’ani tukufu kwa wanaume nchini Uingereza kwa mara ya kwanza, chini ya usimamizi wa taasisi ya Imamu Khui iliyopo Landan na wameshiriki wasomaji wa Qur’ani kutoka miji tofauti ya Uingereza.

Idara ya Maahadi iliunda kamati ya majaji iliyokua na wajumbe wafuatao: Sayyid Ustadh Jalaal Maasumiy, Sayyid Ustadh Haidari Mussawiy, Sayyid Ustadh Haani Wardi na Sayyid Ustadh Nadhiru Hakiim, kwa ajili ya kukagua hukumu za usomaji, uanzaji, usimamaji, sauti na naghma, majaji hao walipasisha jopo la wasomaji kuingia katika mashindano ya Qur’ani, na washindi watatu wakapatikana na kupewa nafasi ya kusoma katika hafla hii iliyo andaliwa na taasisi ya Imamu Khui, mshindi wa kwanza alikua ni Mustafa Ali, na mshindi wa pili ni Yassir Mahadi, na mshindi wa tatu ni Hussein Swaaleh.

Hafla hiyo ilikhutubiwa na Mheshimiwa Dokta Sayyid Fadhili Milani, na ilipambwa na mashairi na kaswida za kumsifu Mtume (s.a.w.w) zilizo ongeza furaha katika nyoyo za wahudhuriaji, na mheshimiwa Sayyid Swahibu Mussawiy ambaye ni mtoto wa Sayyid Khui alizungumza pia, na balozi wa Iraq nchini Ungereza naye alizungumza, pamoja na wanachuoni na wadau wa Qur’ani wanaume kwa wanawake walipewa nafasi ya kutoa michango na maoni yao, hafla hii imehudhuriwa kwa wingi na wahamiaji wa Uingereza, wasomaji waliofaulu wamepewa zawadi pamoja na washiriki wote wa mashindano pia wamepewa zawadi kwa ushiriki wao na kamati ya majaji pia imepewa, sambamba na kuwapa baadhi ya zawadi za kutabaruku kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), wahudhuriaji wameisifu Atabatu Abbasiyya tukufu na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi kwa kuwajali wahamiaji wa kiislamu wanaoishi katika nchi za Magharibi na kuwawekea program za Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: