Hospitali ya rufaa Alkafeel yatibu mamia ya wagonjwa wa miguu iliyo athiriwa na maradhi ya kisukari…

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Imetoa matibabu kwa mamia ya wagonjwa wa miguu iliyo athiriwa na maradhi ya kisukari na kuwapa kinga makumi ya wagonjwa wengine, kupitia kituo cha wataalamu wa magonjwa hayo kwa kutumia Maikrozon na Dairomazon ya maji na Maikrozen ya Haidrojen, dawa hizo zimeonyesha mafanikio makubwa katika nchi nyingi Duniani, hospitali ya rufaa Alkafeel ni msambazaji mkuu wa dawa hizo, na inawataalamu wenye uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi hayo.

Kuathirika miguu ya wenye maradhi ya sukari ni tatizo kubwa kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, kutokana na seli zao kuathiriwa na ugonjwa huo ambao hupelekea kutatiza mzunguko wa damu katika nyayo, Hoapitali ya rufaa Alkafeel inadawa ya kutibu maradhi hayo hatari kwa wanaadamu.

Baada ya kuwatibu na kupona wagonjwa wengi wenye kisukari waliokua wanasumbuliwa na vidonda vya miguuni, imefanikiwa kupunguza wagonjwa wa maradhi hayo hadi kufikia asilimia mbili kwa mia, kutoka asilimia sitini, hali kadhalika tunagawa dawa bure kwa watu wenye kisukari wanaosumbuliwa na vidonda vya miguuni.

Kwa ajili ya kuomba dawa au kupata maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo (07717672301 / 07819434680 / 07730622240) namba hizo zinapatikana kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja Alasiri, pia unaweza kuwasiliana nasi kwa Whatsapp simu namba (07827270312), andika majina matatu ya mgonjwa, mkoa alipo, namba yake ya simu, pia andika shida yako na jina la daktari unayetaka akuhudumie.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: