Taasisi ya wapenzi wa Hussein (a.s) ya kiutamaduni yatoa zawadi kwa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Taasisi ya wapenzi wa Hussein (a.s) ya kiutamaduni imetoa zawadi kwa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Jumanne (26 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (4 Desemba 2018m), zawadi hiyo imetolewa kwa ajili ya kuonyesha kuthamini kazi nzuri zinazo fanywa na maktaba ya Ataba tukufu katika ushiriki wake kwenye kongamano la kielimu na kiutamaduni la kimataifa Twafu la awamu ya kumi, lililofanyika hivi karibuni katika chuo kikuu cha Almustanswariyya cha Bagdad.

Katibu mkuu wa taasisi ya wapenzi wa Hussein (a.s) ya kiutamaduni Ustadh Nasibu Jazaairiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Katika ushiriki wake kwenye kongamano la Twafu lililofanyika hivi karibuni katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya, pembezoni mwa kongamano hilo tulifanya kikao na wasimamizi wa maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tulishuhudia mwitikio mkubwa na tulipata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa watu walio tembelea kongamano hilo, wanafunzi kwa walimu, kutokana na vitu walivyo kuanavyo vilivyo toa picha halisi ya elimu inayo hitajika wakati huu”.

Akaongeza kua: “Tulipata picha wazi kua kazi za Atabatu Abbasiyya tukufu haziishii kwenye kuratibu mambo ya mazuwaru na kuwahudumia peke yake, bali wanaratiba kamili ya mambo ya kielimu inayo endana na mtazamo wa jamii pamoja na utamaduni wa wairaq wote, jambo hili ni zuri sana sisi kama taasisi ya kiutamaduni tumefurahi sana, tunatoa pongezi kubwa kwa maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kazi nzuri wanazo fanya”.

Akamaliza kwa kusema: “Leo tumekuja kutoa shukrani zetu kwa maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tunawaambia kua: hakika sisi tunawapongeza sana na tutafurahi zaidi iwapo ushirikiano baina yetu na Atabatu Abbasiyya tukufu utaendelea kupitia maktaba yake, tulikua hatujui kama Atabatu Abbasiyya inamakta kubwa yenye aina ya vitabu elfu (50) vilivyo wekwa katika mpangilio na utaratibu bora zaidi, tumeshangwazwa na tulicho kiona”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: