Nafasi ya Abulfadhil Abbasi mbele ya baba yake Kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Katika kitabu cha (Qamaru bani Hashim) imeandikwa kua: Ummul Banina (a.s) alimuona kiongozi wa waumini (a.s) amemkalisha mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s) miguuni kwake alipo kua mdogo, akamnyoosha mikono yake na akaibusu kisha akaanza akalia, hali hiyo ilimshitua, na akashangazwa sana, akamsogelea kiongozi wa waumini akamwambia: Mwenyezi Mungu anakuliza ewe kiongozi wa waumini, mikono ya mwanangu inakitu kinacho kufanya ulie?!

Imamu kiongozi wa waumini (a.s) akamsimamisha na kumwambia, mtoto huyu anautukufu mkubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kutokana na yale atakayo fanya kwa ajili ya kumnusuru ndugu yake na Imamu wake Hussein (a.s) siku ya mwezi kumi Muharam, atapambana hadi atakatwa mikono yote miwili.

Mama hakuweza kuvumilia baada ya kusikia maneno hayo alianza kulia, na watu aliokua nao pia wakalia, Imamu kiongozi wa waumini (a.s) akawatuliza na kuwanyamazisha, kisha akamwambia Ummul Banina (a.s) heshima kubwa aliyo nayo mwanae mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, akamwambia kua; baada ya kukatwa mikono yake miwili Mwenyezi Mungu atampa mbawa na ataruka pamoja na Malaika kwenda peponi, kama ilivyo kua kwa Jafari bun Abu Twalib (a.s).

Ni wazi kua Imamu kiongozi wa waumini (a.s) kumbusu mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenye mikono yake sio dalili ya mapenzi peke yake, bali pia ni dalili ya utukufu wake.

Imeandikwa katika kitabu cha Ma’ali Sibtwain kua: Ulipoingia usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani mwaka wa arubaini hijiriyya, siku aliyokufa Imamu kiongozi wa waumini (a.s), ambayo ni siku ya mwisho katika umri wa Imamu kiongozi wa waumini (a.s), alianza kuwaaga watu wa nyumbani kwake na kuwapa usia na mawaidha, akamwangalia mtoto wake Abulfadhil Abbasi (a.s) akamkumbatia kifuani kwake na akamwambia: (Mwanangu Abbasi utakua tulizo la macho yangu siku ya kiyama…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: