Mwezi kumi Rabiul Aakhar ni kumbukumbu ya kifo cha Fatuma Maasuma (a.s)…

Maoni katika picha
Siku kama ya leo –mwezi kumi Rabiul Aakhar- alifariki bibi Fatuma Maasuma bint wa Imamu Mussa Alkadhim na dada wa Imamu Ridhaa (a.s), alifariki tarehe kama ya leo mwaka (201h) katika mji wa Qum, akiwa na umri usiozidi miaka ishirini na nane kama ilivyo kuja katika riwaya, katika umri huo mdogo alipitia mitihani mingi kama shangazi yake Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), alizaliwa baba yake akiwa jela na amesha fanyiwa mateso mengi na utawala wa Abbasiyya, yeye pia alivumilia manyanyaso mbalimbali kutoka kwa watawala wa bani Abbasi.

Safari wake (a.s) ya kwenda Qum

Alikua sawa na watu wengine katika familia ta Abu Twalib, alipata dhiki kubwa katika nafsi baada ya kaka yake Imamu Ridhaa (a.s) kuitwa na Ma-amuun aende Khurasani, na alipata hofu kubwa baada ya kuambiwa na kaka yake kua atafariki katika safari hiyo, akaamua kufunga safari na kumfuata ndugu yake (a.s), akiwa na matarajio madogo ya kukutana nae akiwa hai, kutokana na umbali wa safari pamoja na uchovu aliugua akiwa njiani, akashindwa kuendelea na safari, akauliza umbali wa mahala alipo ugulia na mji wa Qum, hapo alikua katika mji wa Saawah, wakamwambia Qum ipo umbali wa Farsakh (kilometa) 70, akaamrisha apelekwe katika mji wa Qum.

Kuwasili kwake (a.s) katika mji wa Qum

Alibebwa hadi Qum akiwa mgonjwa, alipo wasili alipokelewa na viongozi wa Qum, wakitanguliwa na Mussa bun Khazraji bun Sa’adi Ash’ariy, akashika kamba ya ngamia wake na akampeleka hadi nyumbani kwake, aliishi katika nyumba yake hadi alipo fikwa na umauti, baada ya siku 17 akaamrisha aoshwe, avishwe sanda na kuswaliwa kisha akaenda kuzikwa, mahala ambapo kaburi lake lipo hadi sasa, wakajenga banda juu ya kaburi lake, hadi bibi Zainabu bint wa Imamu Muhammad Jawaad (a.s) alipo kuja kumjengea kubba.

Kifo chake (a.s)

Bibi Fatuma aliishi katika mji wa Qum siku 17, alifanya ibada na kuswali katika nyumba inayo itwa Nyumba yenye nuru (Baitu Nnuur), sasa hivi ipo katika mji wa (Satiih) akafariki mwezi kumi Rabiu Thani, (au mwezi kumi na mbili kwa kauli nyingine) kabla ya kukutana na kaka yake, mazishi yake yalihudhuriwa na watu wengi sana, wakaenda kumzika katika makaburi ya (Babalaan), sehemu ambayo kaburi lake lipo hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: