Katika malalo yake tukufu: Watu wa karbala wanaomboleza kifo cha bibi Fatuma Maasuma (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika kumliwaza Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), kundi kubwa la watu wa mji wa Shahada na undugu Karbala tukufu wamefanya maombolezo ya kifo cha bibi Fatuma Maasuma (a.s) mbele ya kaburi lake tukufu katika mji wa Qum, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu ambacho kipo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Kundi kubwa la wapenzi wa Ahlulbait (a.s) waishio Karbala wamekuja Qum wakitokea miji tofauti wakiwa katika vikundi vya Husseiniyya, wakakusanyika chini ya bendera moja ambayo ni maukibu ya kuomboleza ya watu wa Karbala, kwa pamoja wakaelekea katika malalo ya bibi Fatuma Maasuma (a.s) ndani ya mji wa Qum, maukibu yao ilikua kubwa kushinda maukibu zote zilizo kuwepo katika malalo hayo kwa siku hiyo kuomboleza msiba huu mkubwa kwa wafuasi na wapenzi wa watu wa nyuma ya Mtume (a.s).

Kitengo cha maadhimisho na mawakubu Husseiniyya kiliweka mazingira mazuri na kuondoa kila aina ya ugumu kwa kushirikiana na pande zinazo husika ndani ya mji wa Qum na kuhakikisha maukibi hizo zinaingia na kufanya idaba zao kwa amani na utulivu.

Kumbuka kua katika siku kama ya leo –mwezi kumi Rabiul Aakhar- alifariki Dunia bibi Fatuma Maasuma bint wa Imamu Mussa Alkadhim na dada wa Imamu Ridhaa (a.s) mwaka wa (201h) katika mji wa Qum, akiwa na umri usiozidi miaka ishirini na nane kama ilivyo kuja katika riwaya, pamoja na umri mdogo huo lakini alipitia mitihani mingi kama shangazi yake Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), alizaliwa baba yake akiwa jela, na akiwa amesha nyanyaswa sana na utawala wa Abbasiyya, yeye pia alivumilia manyanyaso mengi kutoka kwa watawala wa bani Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: