Makamo rais wa umoja wa maktaba za kiarabu: Kuzungumzia maktaba katika taifa ambalo ndio msingi wa maktaba ni sawa na kuuza maji mbele ya mto wa Dujla na Furaat

Maoni katika picha
Makamo rais wa umoja wa maktaba za kiarabu Dokta Sefu bun Abdullahi Aljaabiriy alizungumza katika nadwa ya kielimu iliyo andaliwa na chuo kikuu cha Al-Ameed asubuhi ya Jumatano (11 Rabiu Thani 1440h) sawa na (19 Desemba 2018m) iliyokua na anuani isemayo: (Nafasi ya maktaba za udaktari za Iraq katika kufikia malengo ya mpango wa maendeleo endelevu 2030m).

Jaabiriy alianza kuongea kwa kusema: “Kwa jina langu na jina la umoja wa maktaba za kiarabu, ni furaha kubwa kwangu kuwa pamoja nanyi katika kikao hiki kitukufu, kinacho zungumzia nafasi ya maktaba za udaktari kwa malengo ya maendeleo endelevu hapa Iraq, taifa lenye asili ya utukufu, kuzungumzia maktaba katika nchi ambayo ndio msingi wa kuanzishwa kwa maktaba ni sawa na mtu anayeuza maji mbele yamto Dujla na Furaat, lakini sio vibaya kujadili maendeleo ya kisasa na kuangalia mambo yanayo weza kuboresha maktaba zetu na kuzifanya kua bora zaidi kwa watafiti wa maswala ya udaktari”.

Akaongeza kua: “Hakuna shaka kua maktaba zinamchango muhimu katika kufanya utafiti kwenye mambo ya kielimu, hasa tunapozungumzia fani bora zaidi, fani ya udaktari, hakika maktaba zinamchango mkubwa katika kuendeleza na kukuza uwezo wa watumishi wa fani hiyo, sawa wawe madaktari au wasaidizi wao, taasisi za afya zinalipa umuhimu mkubwa swala hili, kwa sababu mtu aliyebobea katika maswala ya maktaba anauwezo mkubwa wa kusambaza elimu yake kwa watu wengine yatupasa kuzingatia swala hili”.

Akaendelea kusema: “Ilipo patikana Intanet na kila kitu kikabadilika kutoka katika ulimwengu wa karatasi na kuingia katika ulimwengu wa elektronik, Dunia ilidhani kua maktaba zitaisha, na uchapishaji wa vitabu utaisha, lakini baada ya miaka kadhaa mambo yamekua tofauti, maktaba bado zipo na uandishi wa nyaraka mbalimbali bado unaendelea na umuhimu wake unaonekana wazi, watu bado wanaendelea kusomea na kuboe katika mambo hayo, kwa hiyo maktaba bado zina nafasi kubwa katika taasisi zote za kiutafiti na kielimu”.

Akamaliza kwa kusema: “Umoja wa maktaba za kiarabu unafanya kila uwezalo katika kuboresha na kuendeleza maktaba pamoja na kuendeleza watumishi wake, kwa kubadilishana uzowefu na kufanya nadwa zinazo endeshwa na wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali Duniani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: