Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu wahudhuria kikao cha kielimu kilicho fanywa na kitivo cha fiqhi katika mji wa Najafu Ashrafu

Maoni katika picha
Katika kuendeleza ushirikiano mwema na watu wa nje pamoja na kuitikia mwaliko walio pewa, ugeni unaowakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu umeshiriki katika kikao cha kielimu kilicho fanywa na kitivo cha fiqhi katika mkoa wa Najafu kilicho kua na anuani isemayo: (Mambo muhimu wanayoshirikiana shia na katoliki na namna ya kupambana na changamoto kati ya pande mbili) kilicho fanyika katika ukumbi wa chuo.

Kiongozi wa ujumbe huo alikua ni Shekh Ammaar Hilali ambaye ni rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu pamoja na kiongozi wa kituo cha maarifa ya Qur’ani kuifasiri na kuichapisha shekh Dhiyaau-Dini Zubaidiy.

Kikao hicho kimehudhuriwa na jopo la makasisi wa kanisa katoliki kutoka Ufaransa pamoja na wajumbe wengine, kikao kilifunguliwa na kiongozi wa kitivo cha fiqhi, baada yake akazungumza dokta Emanuel kutoka Ufaransa ambaye alielezea misingi ya imani ya kanisa Katoliki, kisha dokta Abdul-Amiir Zaahid akazungumzia kuhusu vipengele muhimu wanavyo kubaliana na kutofautiana baina ya pande hizo mbili.

Kikao kilihitimishwa kwa kupokea maoni na maelezo mbalimbali kutoka kwa maustadhi waliobobea, na kilihitimiswa na kauli ya rais wa jumuiya ya Muntada Nnashri –taasisi ya kitivo cha fiqhi- Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: