Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji chaanza kazi ya kuondoa mabaki ya vilipuzi katika mji wa Bartwala na Ba’ashiqa katika jangwa la Nainawa

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza kuanza kazi ya kuondoa mabaki ya vilipuzi viliyo wekwa na magaidi wa Daesh katika wilaya mbili, ya Bartwala na Ba’ashiqa kwenye majangwa ya Nainawa, kikosi cha Abbasi kimeahidi kutumia wahandisi maalumu katika miji tuliyo taja wakiwa na vifaa vya (SCAN JACK AB3500) vyenye uwezo mkubwa wa kutambua vilipuzi hapa nchini.

Jambo hili limefikiwa baada ya ziara waliyo fanya viongozi wa kikosi cha Abbasi katika nyumba ya Shahidi Hussein Abbasi Shabakiy huko Bartwala ambaye alikua mmoja wa wahandisi wa kikosi cha 30 cha Hashdi, na baba wa shahidi huyo akawaomba viongozi hao kuondoa mabaki ya vilipuzi yaliyo wekwa na magaidi wa Daesh katika mji huo, walitembelea kambi ya jeshi ya mji huo na kubaini sehemu ambazo zinavilipuzi.

Tunapenda kukufahamisha kua siku chache zilizo pita msafara wa kutoa misaada chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulikwenda Mosul, ukawatembelea viongozi wa Aizidiy katika mji wa Ba’ashiqa na Ba’azani, waliwajulia hali na kuwapa misaada waliyo hitaji.

Ujumbe huo ulitembelea pia makanisa kadhaa na ukakutana na wafungwa wakristo kama sehemu ya kuimarisha uhusiano wa raia wa Iraq, na kuonyesha kushikamana na watu walioathiriwa na magaidi wa Daesh katika miji hiyo, karibu gari (200) kutoka mikoa tofauti ya Iraq zilibeba vitu mbalimbali na kwenda kuvigawa Mosul kwa wananchi ya kabila la Aizidiy.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: