Uwanja wa haram ya Imamu Ridhaa (a.s) wawa mwenyeji wa maonyesho ya picha za mnato yaliyo ratibiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kwa kushirikiana na ubalozi mdogo wa Iraq katika mji wa Mash-hadi

Maoni katika picha
Kwa mwaka wa pili mfululizo moja ya kumbi za haram ya Imamu Ridhaa (a.s) katika mji mtukufu wa mash-hadi umekua mwenyeji wa maonyesho ya picha za mnato yanayo ratibiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, picha hizo zinahusu maombolezo ya Ashura pamoja na ziara ya arubaini na huduma zinazo tolewa na mawakibu za kuomboleza na za kutoa huduma.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho haya yamefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu) kuna mabango ya picha yapatayo (53), zikionyesha matukio mbalimbali kuhusu maombolezo ya Imamu Hussein ndani na nje ya mji wa Karbala, pamoja na matembezi ya mamilioni ya watu na huduma wanazo pewa katika kipindi cha arubaini iliyo pita”.

Akaongeza kua: “Maonyesho ya mwaka huu yanatofautiana na mwaka jana katika ujumbe wake na madhumuni yake kutokana na kazi nzuri zinazo onyeshwa, mabango ya picha zilizo tengenezwa kwa umaridadi na ustadi wa hali ya juu zimekua kiunganishi kizuri cha mji mtukufu wa Mash-hadi na Ataba takatifu za Karbala”.

Akabainisha kua: “Wakazi wa mji wa Mash-hadi pamoja na mazuwaru wamejitokeza kwa wingi kutembelea maonyesho haya, pamoja na balozi mdogo wa Iraq Ustadh Yasini Sharifu Naswifu, amesifu maonyesho haya na kuomba yafanyike pia katika mikoa mingine ya Iran baada ya kuongezewa vionjo vingine vya matembezi na mapambano ya Imamu Hussein (a.s) ili watu wote waweze kutambua”.

Akamaliza kwa kusema: “Watu walio tembelea maonyesho haya pia wameyasifu na kusema yanaumuhimu mkubwa, kila kitu kilichopo katika maonyesho haya kina upekee wake na kinastahiki pongezi, na wamewashukuru wasimamizi wa maonyesho haya kwa kuwapa fursa ya kufahamu yanayo jiri katika ziara ya Arubaini na huduma wanazopewa mazuwaru watukufu”.

Kumbuka kua maonyesho haya ni moja ya harakati nyingi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa harakati hizo ni kufanya maonyesho ya picha ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, kufuatia tukio lolote la furaha au huzuni linalo husu maimamu wa Ahlulbait (a.s), sambamba na vitendo vya watu wanaokwenda kutembelea malalo tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: