Abulfadhil Abbasi (a.s) na utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingelifanya hayo ila wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeli fanya walio waidhiwa ingeli kuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi * Na hapo tunge wapa malipo makubwa kutoka kwetu * Na tungeli waongoa njia iliyo nyooka * Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema, na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao! * Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kutosha).

Miongoni mwa misdaaq (matokeo) ya aya hizi tukufu ni mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Shahidi wa Karbala Imamu Hussein (a.s) na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Mwenyezi Mungu mtukufu amesha mwandikia mjukuu wa Mtume wake na wasii wa wasii wake Imamu Hussein (a.s) kua; atahama na kuuwawa, na kwamba atapambana na Yazidi amabaye ni adui wa Mwenyezi Mungu na adui wa Mtume wake, na akamwambia kipenzi chake Mtume (s.a.w.w) aliyo mpangia mjukuu wake kupitia Malaika Jibrilu (a.s), Imamu Hussein (a.s) akatekeleza amri ya Mola wake akatoka kupambana na Yazidi, hawakutoka pamoja nae ispokua watu wachache, miongoni mwa watu hao wachache ni Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hakika (a.s) alifanya kila alilo ambiwa na kila analo tambua, alikua mtu mwema kwake, alipata malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, na aliongozwa katika njia iliyo nyooka, hakika atafufuliwa kama ilivyo kuja katika ziara yake iliyo pokelewa na Imamu Swadiq (a.s) namna alivyo mtii Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Imamu wake pamoja na walioneemeshwa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na Masiddiqi, na Mashahidi, na Waja wema, na hao ndio marafiki bora zaidi, hakika alisadikisha (a.s) na akathibitisha kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kutosha).

Hongera kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) anahadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hongera kwake kwa nafasi kubwa aliyo nayo!
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: