Kituo cha faharasi na kuratibu elimu kinaendesha semina kwa wasomi wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Karbala

Maoni katika picha
Kutokana na kauli ya kiongozi wa waumini Ali (a.s) isemayo: (Zaka ya elimu ni kuifundisha), na kutokana na mwenendo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuwafundisha raia wa Iraq elimu mbalimbali, na kutokana na uwezo mkubwa walio nao watumishi wa kituo cha faharasi na kuratibu elimu chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat wa kutumia program ya faharasi, ambayo ni program ya kimataifa kwa sasa inatumiwa na maktaba nyingi Duniani, wameandaa semina kwa watumishi wa kitivo cha uhandisi (RDA) katika chuo kikuu cha Karbala, kufuati ombi walilo toa la kutaka kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wao wa maktaba, kutokana na ujuzi mkubwa walionao watalamu wa Ataba tukufu katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Hassanaini Mussawiy: “Semina itafanyika kwa muda wa siku nane, mafunzo yamewekwa sehemu mbili: sehemu ya nadhariyya, inahusisha faharasi ya sifa na faharasi ya maudhui pamoja na sehemu ya sanadi, na sehemu ya pili ni ya vitengo, baada ya kuwafundisha kwa nadhariyya wiki nzima, kisha wakafundishwa kwa vitendo namna ya kuingiza taarifa kwa kufuata kanuni za kisasa”.

Kumbuka kua semina hii ni moja ya semina nyingi zinazo kusudia kujenga uwezo na kusambaza zaidi elimu hii, na kurithisha wengine uzowefu na ujuzi katika sekta hii, na kuongeza wataalamu wa program ya faharasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: