Tambua sehemu muhimu zinazo pewa maji safi ya kunywa na idara ya maji ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mkuu wa idara ya maji katika kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Ahmadi Jaasim Hanuun amesema kua; Idara ya maji inaendelea kugawa maji safi ya kunywa katika maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na hali ya hewa kuwa ya baridi, kazi hii inaendelea kufanywa na watumishi wa idara ya maji bila kusimama, wanagawa maji kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumfanya mnyweshaji wa maji kua kiigizo chao.

Sehemu wanazo sambaza maji ni:

  • 1- Sehemu zote ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile shule za Al-Ameed, vituo vya ulinzi na usalama, vituo vyote vya ukaguzi vilivyo chini ya walinzi wa haram mbili tukufu, vitalu vya Alkafeel ambavyo ni vitatu (3), bwawa la samaki la Alkafeel, maegesho ya magari (maegesho/90, maegesho/39, maegesho/47 na maegesho/49) pamoja na maegesho ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi, na chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Ataba tukufu, kituo cha kitengo cha miradi, pamoja na kusambaza maji katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na katika kiwanda sa Saqaa cha kutengeneza madirisha (ya makaburi).
  • 2- Tunasambaza maji safi ya kunjwa kwenye shule zaidi ya (20) zilizo chini ya idara ya malezi ya mkoa wa Karbala chini ya utaratibu maalum.
  • 3- Tunasambaza maji safi ya kunywa katika baadhi ya vijiji na miji inayo zunguka mkoa wa Karbala pamoja na maeneo ya kilimo (mashambani).
  • 4- Tunasambaza maji safi ya kunywa katika baadhi ya nyumba za makazi, kama vile nyumba za Abbasi (a.s) na zinginezo zinazo ishi watu.
  • 5- Tunashiriki kikamilifu katika kumbukumbu ya kifo au kuzaliwa Imamu yeyote miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Bagdad, Najafu na Samaraa sambamba na kugawa maji safi ya kunywa kwa mazuwaru na mawakibu pamoja na kugawa vipande vya barafu katika majira ya joto.
  • 6- Huandaa maji safi ya kunywa kwa ajili ya mahujaji wanaotumia barabara kwa muda wa siku (15) hadi msafara wa mwisho wa mahujaji urudi kutoka katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.
  • 7- Huandaa maji safi ya kunywa na barafu katika matukio yote yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile tukio la igizo la Twafu ambalo hufanywa katika barabara ya Najafu na mengineyo.
  • 8- Tunagawa maji safi ya kunywa kwa wakazi na mazuwaru kila siku kupitia vituo viwili, kituo cha Hauraa Zainabu (a.s) na kituo cha Aljuud.

Kumbuka kua idara zote na ofisi mbalimbali zinazo fanya kazi chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya zinafanya kazi usiku na mchana, kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: