Kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Husomwa Duaau Komaili katika kila usiku wa Ijumaa kwa sauti nzuri

Maoni katika picha
Kama inavyo julikana; waumini wa ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala kila siku ya Alkhamisi huelekea katika malalo ya Sayyid Shuhadaau na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamezowea kuja kufanya ibada za usiku wa Ijumaa pamoja na ziara katika eneo hilo takatifu, na kutokana na utukufu wa usiku wa Ijumaa, utawaona wanafanya ibada mbalimbali katika eneo hilo tukufu, miongoni mwa ibada hizo ni kuswali swala ya Magharibi na Isha kwa jamaa kisha hukusanyika na kusoma dua iliyopokewa kutoka kwa kiongozi wa waumini aliyo mfundisha Komaili bun Ziyadi inayo itwa (Duaau Komaili).

Kila usiku wa Ijumaa husomwa duaau Komaili katika sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s), sehemu ya pili ni uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na sehemu ya tatu ni ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na wingi wa mazuwaru wanaokuja kusoma duaau Komaili, kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kimeandaa sehemu na mimbari kwa ajili ya kusoma dua hii tukufu, kwa ajili ya kuondoa usumbufu na kuhakikisha usomaji wa dua hiyo hauwi kikwazo kwa mazuwaru wengine katika utendaji wa ibada zao.

Msomaji mashuhuri bwana Ali Ka’abiy hupanda katika mimbari na kusoma dua kwa sauti nzuri ambayo hufurahisha nyoyo za wasomaji wengine wa duaau Komaili, na huenea mazingira mazuri ya kiroho kwa mazuwaru na utawaona wanainua mikono yao juu kwa unyenyekevu, wakijikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mkutufu wakiwa karibu na kaburi la walii wake na mja mwema aliyekatwa mikono miwili Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: