Katika mazingira yaliyojaa furaha ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanyika hafla ya kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, Alasiri ya Jumamosi (5 Jamadal Uula 1440h, sawa na 12 Januari 2019m), imefanya hafla ya kusherehekea kuzaliwa kwake, kwani alizaliwa tarehe kama ya leo mwezi tano Jamadal Uula.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ilipambwa na kaswida za kimashairi pamoja na tenzi mbalimbali kutoka kwa washairi mahiri zilizo konga (furahisha) nyoyo za wahudhuriaji, tenzi zilikua na maudhui ya kuelezea utukufu wa bibi Zainabu (a.s), mtu ambaye jina lake limehifadhiwa katika historia kwa herufi za dhahabu, hali kadhalika wakaonyesha mapenzi yao na namna wanavyo shikamana na Mtume pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), wakasisitiza kua kumbukumbu hii iwe chachu ya mshikamano na kuunga undugu kati ya waislamu wote, hususan wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Kumbuka kua bibi Zainabu (a.s) alizaliwa mwezi tano Jamadal Uula mwaka wa sita hijiriyya, ndipo nuru yake alipo angaza duniani na kuingiza furaha katika katika moyo wa baba yake Ali bun Abu Twalib na mama yake mbora wa wanawake wa duniani Zaharaa (a.s), alikua mwingi wa kufanya ibada, ujuzi, mwenye zuhudi (kuipa nyongo dunia), kwa nini asiwe hivyo wakati yeye ni mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) aliye lelewa na miguu bora ya Ali na Fatuma (a.s), alichota katika bahari ya elimu zao na elimu za kaka zake mabwana wa vijana wa peponi Hassan na Hussein (a.s).