Kwa huduma za pekee: Msafara wa Saaqi umetangaza kuanza usajili wa kwenda Umra katika mwaka huu wa 1440h

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia msafara wa Saaqi, imetangaza utaratibu maalumu wa safari ya Umra na kuzuru kaburi la Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Maimamu wa Baqii (a.s) na sehemu zingine takatifu katika mji wa Maka na Madina, imetowa wito kwa wanaotaka kwenda Umra wafanye haraka kusajili majina yao.

Utaratibu wa safari unahusisha:

  1. Fiza.
  2. Usafiri wa kisasa.
  3. Milo mitatu kipindi chote cha safari.
  4. Makazi katika hoteli nzuri, siku nne katika mji wa Madina na siku sita katika mji mtukufu wa Maka.

Kwa kujisajili na maelezo zaidi tembelea ofisi za idara zifuatazo:

Ofisi ya kwanza / ipo katika eneo la Mlago wa Bagdad- hoteli ya Jazira ya zamani- karibu na kituo cha Alqamar.

Ofisi ya pili / ipo katika eneo la Mlango wa Kibla kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Au piga moja ya namba zifuatazo: 07801952463 / 07602326779 / 07602327074.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: