Wataalamu wa kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel watoa matibabu ya meno bure kwa watu zaidi ya (200) kila siku

Maoni katika picha
Kufuatia huduma zake za kibinaadamu katika sekta mbalimbali, na kutokana na uchache wa vituo vya afya vinavyo jihusisha na tiba ya meno hapa Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitivo cha tiba ya meno katika chuo kikuu cha Alkafeel kwenye mkoa wa Najafu, kinacho toa tiba na kinga ya maradhi ya meno wakitumia vifaa tiba vya kimataifa chini ya kamati ya madaktari bingwa wa meno.

Tumeongea na mkuu wa chuo cha Alkafeel Dokta Nursi Muhammad Dahhaani amesema kua: “Kitengo cha udaktari wa meno kimekua na kesi (wagonjwa) wengi wa umri tofauti, kutokana na uwezo mkubwa walionao madaktari wake unao onekana katika kazi wanazo fanya, wameaminiwa na wagonjwa wa meno wa aina zote”.

Akaongeza kua: “Tunapokea zaidi ya wagonjwa (200) na kuwatibu bure kila siku, hii ni ishara nzuri, na idadi inaendelea kuongezeka, inaonyesha wazi namna wagonjwa walivyo na imani kubwa na madaktari wao”.

Kuhusu vifaa tiba vinavyo tumika katika kitivo cha udaktari wa meno kwenye chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Mahdi Karim amesema kua: “Vifaa tiba vinavyo tumika vinaubora wa kimataifa na vimepasishwa na wizara ya afya ya Iraq, kwa ajili ya kuhakikisha tunafikia malengo kwa ufanisi wa hali ya juu na kupata matokeo mazuri, jambo hili limefikiwa katika miaka ambayo tumekua tukitoa huduma hii”.

Naye Dokta Khaludu Swafi kutoka kitivo cha udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel amesema kua: “Wanafunzi wetu wanatumia vifaa tiba vya kisasa zaidi ambayo hununuliwa na kamati maalumu ya chuo, ambavyo ni vifaa bora zaidi kimataifa, hii ni kwa ajili ya maslahi ya mwanafunzi na mgonjwa, tunamsimamia mwanafunzi kuanzia hatua ya kupekea mgonjwa hadi hatua ya mwisho, na tunampa vifaa vyote vinavyo hitajika katika hatua hizo, huwa tunamwachiwa mwanafunzi amalizie hatua ya nne na ya tano chini ya uangalizi wa karibu zaidi wa wakufunzi bingwa wa udaktari wa meno, nao huwa ni wanafunzi waliofauli kwa viwango vya juu kabisa, huchukuliwa na kutumiwa na chuo chetu”.

Dokta Rihabi Abdulhussein Ali ameongea kuhusu matubabu ya watoto kua: “Tunatoa umuhimu mkubwa sana kuhusu tiba za watoto, kama mnavyo jua mtoto anahitaji kuandaliwa kisaikolojia unapo muhudumia, sisi tunajitahidi kumfanya ajiamini pamoja na kuwajengea imani wazazi wake wakati tunapotoa huduma, kisha huwa tunachagua aina bora ya kumtibu, sio kutibu maradhi aliyonayo tu bali pamoja na kumpa kinga kwa ajili ya maradhi anayoweza kuyapata baadae”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: