Shughuli za kongamano la Shahada ambalo hufanyika kila mwaka zimeanza

Maoni katika picha
Katika awamu yake ya nane na chini ya kauli mbiu isemayo: (Msimamo wa bibi Zaharaa ni mnara wa imani za watu huru), shughuli za kongamano la Shahada la wanawake ambalo husimamiwa na Muntada Imamu Hussein (a.s) ya kitamaduni na ofisi ya Mawakibu Husseiniyya katika wilaya ya Dabuni kwenye mkoa wa Waasit kwa kushirikiana na Ataba tukufu zimeanza, kwa ajili ya kuhuisha na kukumbuka kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na mashahidi wa Iraq walio uwawa kwa sababu ya kulinda taifa hili tukufu.

Hafla ya kongamano hilo imepata mahudhurio makubwa wakiwemo viongozi wa dini na wawakilishi wa ofisi za Maraajii Dini watukufu, na ugeni uliowakilisha Ataba tukufu, na wawakilishi mbalimbali wa Maraajii katika mkoa wa Waasit pamoja na viongozi wa kikoo, bila kusahau familia za wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na wakazi wa wilaya ya Dabuni na vitongoji vya jirani yake.

Baada ya kusoma Qur’ani ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, Mkuu wa ofisi ya malezi ya Aziziyya alizungumza na akasisitiza kuhusu: “Umuhimu wa kuamiliana na dhulma alizofanyiwa Zaharaa (a.s) kimalezi, na kuziangazia katika selebasi zetu za masomo, kwa sababa dhulma hizo zinatupasa kuchukua msimamo sio wa maneno tu bali wa vitendo, kwa sababu tunahitaji kila kauli aliyo itamka na kila jambo alilofanya kwani yeye ndio kiigizo chetu”.

Yakafuata mawaidha ya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Shekh Swalehe Qarah Ghuli ambaye alifafanua: “Namna Mtume (s.a.w.w) alivyokua akiamiliana na Zaharaa (a.s), kuamiliana kwao ni somo kwa umma aliokuja kuuongoza usipotee, kongamano hili ni ujumbe tunaotuma kwa Imamu Hujjah (a.f) ya kwamba sisi tunatekeleza ahadi ya Mtume (s.a.w.w)”.

Kisha ukafuata ujumbe wa mwongozo na malezi (Tarbiyya wa Irshaadi) ulio wasilishwa na Mheshimiwa Alammah Sayyid Ahmad Ashkuri ambaye amebainisha kua: “Hakika watu wapo makundi makundi, kundi la kwanza ni lile linalo ona njia ya haki na linaifuata hata kama itawagharimu sana, maadam amesha bainikiwa na njia ya haki na kujua mwongozo basi anashikamana nayo hadi afike katika haki, hao ndio wenye mtazamo sahihi na wanautambuzi, wanajua wapi wanakwenda wanavumilia na wako tayali kujitolea kila kitu. Kundi la pili la watu ni wale ambao wanaona njia ya haki lakini hawataki kuifuata, wanatambua njia ya haki na wanaiona lakini hawaifuati, wala hawataki kuitegemea, hakika mradi wa Fatuma (a.s) unaweza kua na pande mbili, upande mmoja unaweza kua mradi wa kuongoza na kuwafaidisha watu wenye imani wenye malengo fulani, na upande wa pili ni watu wenye chuki, nao wanafanya juhudi ya kushusha utukufu wa Fatuma (a.s), na kufanya mradi wa kueneza chuki na wala sio mradi wa kuongoza watu, Fatuma (a.s) ni mtu asiyekua na mfano, Mwenyezi Mungu ametaka akumbukwe daima sio kwa muda mfupi tu, alishambuliwa mara ya pili kwa kushusha utukufu wake na kupewa mtu mwingine”.

Kongamano limepambwa na kaswida za kimashairi kuhusu bibi Zaharaa (a.s) na dhulma alizo fanyiwa baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), kulikua na tenzi za kuomboleza pamoja na maigizo yaliyo fanywa na kikosi cha Nnabaa Al’adhiim lililo pewa jila la (Kuingia nyumba).

Hafla ikahitimishwa kwa kugawa midani na vyeti kwa baadhi ya viongozi walio hudhuria, pia kugawa zawadi za pesa za vinginevyo kwa familia (85) za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, zawadi hizo zimetolewa kwa jina la Atabatu Abbasiyya tukufu.

Vilevile katika kongamano hilo kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kimefanya maonyesho ya vitabu, kwa kuonyesha vitabu mbalimbali na majarida, maonyesho hayo yamefanyika siku tatu, kila aliye tembelea katika maonyesho hayo ameyasifu na kuomba yafanyike tena siku zijazo kutokana na umuhimu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: