Vituo vya usambazaji wa vitabu na maktaba za Karbala wanaonyesha bidhaa zao katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Kuna mambo mengi yamefanyika katika msimu wa huzuni za Fatwimiyya yanayo simamiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ambayo yameanza kufanyika siku kadhaa zilizo pita, miongoni mwa mambo hayo ni kupokea vituo vya usambazaji wa vitabu na maktaba za Karbala, kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya vitabu ya Karbala kwenye uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, nafasi yake inaonekana wazi kupitia matawi yanayo shiriki katika maonyesho, wanaonyesha machapisho tofauti ya kidini na kitamaduni, pia ni nifursa ya kuongeza maarifa kwa mazuwaru na kunufaika kwa tukio hili la kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu bwana Riyaadh Ni’imah Salmaan ametuambia kuhusu uhusiano uliopo kati ya kitengo hicho na vituo vya usambazaji wa vitabu na maktaba za Karbala kwa ajili ya ushiriki mzuri, ameongea kua: “Maonyesho ya vitabu ni miongovi mwa mambo muhimu katika msimu wa huzini za Fatwimiyya, pia kwa ajili ya kuendana na tukio hili pamoja na kuhakikisha tunanufaika nalo, tulifanya mkutano mkubwa pamoja na maktaba na vituo vya usambazaji vya Karbala vinavyo shiriki, katika kikao hicho tukakubaliana mada zitakazo tolewa wakati wa maonyesho”.

Akaonyeza kua: “Baada ya hapo ikatengenezwa kamati ya mashekhe katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo kua na jukumu la kuchagua mada zinazo faa kuwasilishwa kwenye maonyesho, zinazo endana na ukubwa wa tukio ambalo limepelekea kufanyika maonyesho haya, kuna vitabu vya aina mbalimbali vinavyo onyeshwa, vitabu vya mafundisho ya dini na vinavyo mzungumzia bibi Zaharaa (a.s) pamoja na vitabu vya Aqida na maarifa mengine ya dini”.

Akaendelea kusema: “Kila mtu anajua wingi wa maktaba katika mji wa Karbala na umuhimu wa kinacho onyeshwa, na mwitikio mkubwa uliopatikana katika maonyesho kipindi hiki cha huzuni za Fatwimiyya ni dalili nzuri juu ya jambo hili”.

Kuhusu mazingira yaliyo andaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya ya kuwawekea wepesi wanaoshiriki katika maonyesho amesema bwana Salmaan kua: “Tumerahisisha uingiaji wa vitabu na kuviweka katika maonyesho, sambamba na kuratibu ukaaji wa washiriki na kuwapa misaada mingine ya kimkakati ambayo kitengo kiliahidi kuitekeleza kwa vituo vya usambazaji wa vitabu na maktaba kwa ajili ya kufanikisha maonyesho haya”.

Upande wa watu wenye maktaba na vituo vya usambazaji wa vitabu, wamekishukuru kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa kuwapa fursa hii tukufu, ya kuja kuonyesha machapisho na vitabu walivyo navyo na kuwarahisishia mambo mengi ambayo yamekua chachu ya kufanikiwa maonyosho haya kwa faida ya maktaba pamoja na vituo vya usambazaji wa vitabu na mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: