Taasisi ya Jawadaini ya Qur’ani katika ugeni wa Arshu Tilaawah

Maoni katika picha
Kufuatia utaratibu wa kukaribisha taasisi za Qur’ani kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala katika mahfali za usomaji wa Qur’ani, imekaribishwa taasisi ya Qur’ani ya Jawadaini kutoka mkoa wa Diwaniyya katika mahfali ya Arshu Tilaawah ambayo hufanywa kila wiki ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kushiriki wasomaji mahiri.

Wamesoma Qur’ani tukufu kwa sauti murua zilizo burudisha masikio ya wahudhuriaji na kusisimua nyoyo walipo ungana na wasomaji wenzao pamoja na mazuwaru katika kikao kikubwa cha usomaji wa Qur’ani tukufu, yakatanda mazingira ya kiroho kwa kukutana utukufu wa Qur’ani na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), walioshiriki katika usomaji ni:

Msomaji Muhammad Ridhwa Salmaan / kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Msomaji Abdullahi Zuhairi Alhusseiniy / kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu –tawi la Hindiyya na mmoja wa wasomaji wa semina ya usomaji wa Qur’ani.

Msomaji Swafaau Ka’abiy / kutoka taasisi ya Qur’ani ya Jawadaini katika mkoa wa Diwaniyya.

Ali Muhammad Najmu / kutoka katika mradi wa kiongozi wa wasomaji.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya inatekeleza miradi mingi ya Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, nao unalenga kunufaika na vipaji vya usomaji wa Qur’ani walivyo navyo vijana na Iraq na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kulea vipaji hivyo katika utaratibu maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: