Waziri wa afya na mazingira: Hospitali ya rufaa Alkafeel ni kituo kikubwa cha matibabu na inatoa mchango mkubwa katika sekta ya afya hapa Iraq

Maoni katika picha
Waziri wa afya na mazingira wa Iraq Dokta Alaa Abduswaahibu Alwaani amesema kua: “Hosputali ya rufaa Alkafeel ni kituo kikubwa cha matibabu na inatoa mchango mkubwa sana katika sekta ya afya hapa Iraq, imeingiza hapa nchini vifaa tiba bora zaidi vyenye viwango vya kimataifa, vinavyo iwezesha kufanya upasuaji wa aina zote, wakati siku za nyuma kuna baadhi ya upasuaji ilikua lazima uende nje ya nchi, imewasaidia wananchi wa Iraq kwa kiasi kikubwa”.

Ameyasema hayo katika ziara aliyo fanya Mheshimiwa waziri kwenye Hospitali hiyo pamoja na ujumbe aliofuatana nao kuangalia huduma zinazo tolewa na Hospitali hiyo, kisha akasema: “Ziara yetu katika hospitali ya Alkafeel ni kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu zinazo tolewa kwa wananchi, kupitia madaktari wa kigeni na wazawa wenye uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji wa aina mbalimbali”.

Mkuu wa Hospitali Dokta Muhammad Azizi aliye fuatana na Mheshimiwa waziri katika ziara hii na kutoa maelezo kuhusu vifaa tiba walivyo navyo na huduma wanazo toa, amesema kua: “Ziara hii ya Mheshimiwa waziri ni miongoni mwa ziara muhimu ambazo watendaji wa serikali wanakuja kuona wenyewe huduma zinazo tolewa na hospitali yetu kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa wenye uzowefu mkubwa, Mheshimiwa waziri ameridhishwa na huduma zinazo tolewa tena kwa kiwango cha juu kabisa, ameahidi kua wizara ipo tayali kusaidia kitu chochote kinacho hitajiwa na Hospitali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: