Maoni katika picha
Sayyid Swafi amekutana na jopo la wazee wa ukoo wa Bani Ka’abi kutoka mkoa wa Waasit katika ukumbi wa utawala ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambapo amesema kua: “Namshukuru Mwenyezi Mungu hakika ukoo wenu -sawa na koo zingine za wairaq- mna mashahidi, mmejitolea kwa hali na mali katika kukomboa taifa hili, hii ndio desturi tukufu ya koo za wairaq zimekua na msimamo wa kupambana na magaidi wa Daesh, sawa iwe kwa kutoa watoto wao au misaada, kama ambavyo hatuwezi kusahau nafasi ya koo hizo -ukiwemo ukoo wenu- katika kuhuisha maadhimisho ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akabainisha kua: “Katika siku za vita dhidi ya magaidi wa Daesh wana koo kupitia mawakibu Husseiniyya walifanya kazi kubwa ya kutoa huduma tukufu kwa wapiganaji, kutokana na huduma walizo wapa ndugu zao wapiganaji ziliwapa nguvu na kuwafanya wapate ushindi, tabia hii inatokana na malezi yanayo patikana katika mimbari za bwana wa Mashahidi (a.s)”.