Vipengele muhimu alivyo zungumza Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (2 Jamadal Aakhar 1440h) sawa na (8 Februari 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameongelea vipengele vingi muhimu vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi hivi sasa, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kuna mambo yapo katika elimu ya jamii, na elimu ya maadili, na katika mazingira ya kitamaduni.
  • - Tunapo ongea kuhusu jamii yetu, hujivunia na tunaweza kubaki na majivuno halafu tukapata faida ndogo.
  • - Kufahamu tatizo ni dalili ya kuweza kulitatua.
  • - Baadhi ya wakati watu wengine hawaoni tatizo, kila utakavyo watahadharisha hawata kusikiliza.
  • - Kuna baadhi ya watu hutaka mafanikio bila kuyatafuta, wanataka kufanyiwa mambo na wengine, yakiwa mazuri wanashukuru, na yakiwa mabaya analaumu, jambo hilo sio sahihi.
  • - Kutokana na mapenzi yetu kwa jamii tunahisi kuna mpasuko, mpasuko huo unasababu nyingi ambazo zinaweza kurekebishwa kwa namna tofauti.
  • - Hakuna sababu moja ya mpasuko pia hakuna njia moja ya kuondoa mpasuko.
  • - Yatupasa kujikumbusha watu muhimu wanao unda familia na wanaowajibika kwenye familia.
  • - Anaye fanya kazi ya malezi na kufundisha anatakiwa ajue majukumu yake.
  • - Malezi yanayo patikana shuleni ni jambo la kawaida kuonekana athari yake ndani ya jamii.
  • - Miongoni mwa matatizo makubwa ni pale mtu anayefanya kazi katika sekta ya limu anapo kua hajui nafasi yake.
  • - Mtu asiye jitambua hawezi kupata mafanikio mazuri.
  • - Kazi ya malezi na elimu ni miongoni mwa kazi bora zaidi.
  • - Jamii inapo amiliana na mtu anayefanya kazi katika sekta ya malezi na elimu inatakiwa ionyeshe utukufu wake.
  • - Elimu ni jambo tukufu katika kila jamii.
  • - Anaefanya kazi ya malezi na elimu anatakiwa ajuwe kua anajukumu kubwa.
  • - Mwalimu anapo mshajihisha mwanafunzi wake kughushi, mwalimu huyo anakua amefanya jambo baya mno kwa jamii.
  • - Hatukubali kuwa na mwanafunzi aliyezowea kughushi kwa sababu atafanya hivyo kwa watoto wetu.
  • - Mtu huvuna alicho panda.
  • - Msimtenganishe mwalimu na mwanafunzi wake.
  • - Mwalimu anatakiwa awe na haiba kwa wanafunzi wake.
  • - Mwalimu akikosa haiba kwa wanafunzi wake atapoteza uaminifu na akipoteza uaminifu kazi inaharibika.
  • - Lazima wawepo watu wema katika jamii na huanza kupatikana kwenye hatua hii.
  • - Familia inatakiwa kufuatilia maendelea ya mtoto wao awapo shule na sio kuacha jukumu lote kwa walimu.
  • - Sio sekta ya elimu peke yake ndio inayo wajibika, mzigo unaweza kua mkubwa kwake.
  • - Sekta ya malezi na elimu zinapo panda megu nzuri kwa vijana tutapata jamii bora.
  • - Mwalimu anahaki ya kuandaliwa mazingira bora.
  • - Mwalimu hatakiwi kuacha kutimiza majukumu yake, uzembe wake huathiri jamii.
  • - Yatupasa kuhakikisha watoto wetu wanapata malezi na elimu sahihi.
  • - Mzazi akizembea pengo lake linaweza kuzibwa na mwalimu katika maswala ya kielimu.
  • - Mwalimu anatakiwa arudishe uaminifu kwake, na kama tukirudisha uaminifu litakua jambo la kheri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: