Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba yake ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu inayo sema kua alifariki mwezi tatu Jamadal Thani, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala na kuhudhuriwa na watumishi wake pamoja na idadi kadhaa ya mazuwaru.

Baada ya Qur’ani tukufu ya ufunguzi ulifuata muhadhara kuhusu bibi mtakasifu mwenye msiba huu, uliotolewa na Sayyid Ahmadi Twawirijawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alianza kwa kukumbusha utukufu wa Ahlulbait (a.s), walikua ni nuru chini ya arshi ya Mwenyezi Mungu wanamsabihi na kumsifu Allah (s.w.t), kisha akaanza kumuelezea bibi Fatuma Zaharaa (a.s), akataja utukufu wake na sifa zake, na akataja baadhi ya hadithi zinazo mzungumzia, na yaliyo mtokea kiongozi wa waumini Ali (a.s) katika siku kama hii, kwa kuondokewa na Zaharaa (a.s), ambae kwa kifo chake ikawa imevunjika nguzo ya pili katika nguzo mbili alizo husia Mtume (s.a.w.w) ambazo ni yeye mwenyewe na binti yake (a.s).

Kisha akaongea mada nyingine, akamtambulisha ni nani Fatuma? Kadri tutakavyo lia na kuomboleza hatuwezi kumpa haki anayo stahiki, kwani kama anavyo sema Mtume (s.a.w.w): “Mwanangu ameitwa Fatuma kwa sababu Mwenyezi Mungu mtukufu amewatenga wafuasi wake na wapenzi wake na moto wa jahannamu siku ya kiyama, hatujui siri alizo pewa na Mwenyezi Mungu, tunapo muomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kusema: Ewe Mola kwa haki ya Fatuma na baba yake na mume wake na watoto wake na siri iliyopo kwake, ni siri gani iliyopo kwake? Hatujui, ni sawa na mtu anaekwenda baharini na kuchota maji kidogo, huyu ndio Zaharaa ni bahari isiyo kauka”.

Akafafanua kua: “Hakika Zaharaa hakuna anaye mjua ispokua Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wasii wake, hao wanajua utukufu wake na siri iliyopo kwake, sisi hatujui anasiri gani, lakini baadhi ya siri hizo hudhihirishwa kwetu, aliumbwa kabla Mwenyezi Mungu hajaumba mbingu na ardhi, imepokewa katika hadithi Kisaa, walipokaa Mtume na Ali na Fatuma na Hassan na Hussein (a.s) chini ya shuka, Mwenyezi Mungu aliwaambia nini Malaika? Alisema: Mimi nimeumba mbingu na kila kitu kwa ajili yao. Adam aliumbwa kabla ya mbingu na aliumbwa kwa udongo, Mwenyezi Mungu mtukufu anamwambia Mtume (s.a.w.w): Mimi sikuumba ulimwengu ispokua ni kwa ajili yako, na kama sio Ali nisinge kuumba na kama sio Fatuma nisinge muumba Ali, hawa Maimamu wetu ndio siri ya uwepo, Mwenyezi Mungu ameumba kila kitu kwa ajili ya hizi nuru tano zilizokua chini ya arshi yake”.

Akamaliza muhadhara wake kwa kutaja tukio na riwaya ya kifo chake (a.s), na namna alivyo zikwa na kiongozi wa waumini (a.s), amani iwe juu yake na juu ya baba yake na mume wake na watoto wake katika siku hii tukufu, siku ya kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: