Balozi wa Hispania nchini Iraq: Karbala ni mfano kwa kila muiraq, Marjaa Dini mkuu ni mlinzi wa amani ana nafasi ya pekee katika kulinda umoja…

Maoni katika picha
Mheshimiwa Khawan Khose Skobar Balozi wa Hispania nchini Iraq ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), wakazungumza mambo mbalimbali, Balozi alibainisha kua: “Mji mtukufu wa Karbala ni mfano bora kwa kila muiraq, mimi ninafuraha sana kuutembelea mji huu na nilifanya ziara kama hii katika mji wa Najafu Ashrafu”.

Akaongeza kua: “Hakika Marjaa Dini mkuu ana nafasi kubwa sana katika kulinda taifa na umoja wa wananchi, alitoa nasaha nzuri kwa wanasiasa wa Iraq, zinazo jenga mustakbali mwema wa taifa, Hispania pia ilitoa mchango katika kuwaangamiza magaidi wa Daesh, tunategemea kujenga uhusiano mkubwa wa kiuchumi na Iraq katika sekta zote, tunaweza kuleta mashirika yetu katika mkoa huu kwa ajili ya kufanya miradi ya kiuchumi kwa manufaa ya pande mbili bila hofu yeyote”.

Sayyid Swafi alimwambia Balozi baada ya kumkaribisha kua mji huu ajihisi ni mji wake, akafafanua kua: “Tunatami ziara hii isiwe ya mwisho katika mji huu, Karbala ni kielelezo muhimu cha kiislamu sio kwa Shia peke yake bali kwa waislamu wote, ni mji wenye historia ya zaidi ya miaka (1420) takriban, na historia yake ya kimazingira ilikuwepo kabla ya kipindi hicho, lakini ulipata utukufu (umaarufu) baada ya kuuwawa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watu waliishi katika mji huu tangu zamani kwa sababu upo karibu na maji, ilikua ni ardhi nzuri kwa kilimo kabla ya kuchukuliwa kua ardhi tukufu kidini, nao ni mji mzuri sana, lakini haukupewa umuhimu unaofaa (na tawala zilizo pita) kwa sababu za kisiasa, tunajitahidi kuuweka katika hadhi yake siku zijazo”.

Akaongeza kua: “Iraq inategemea kupata ushirikiano mzuri kutoka nchi marafiki, Iraq inafursa nyingi katika sekta ya uchumi na kuweka ushirikiano mwema na nchi zingine, kwa bahati mbaya vyombo vya habari vimekuza mno taarifa za ugaidi kwa kiasi vimeingiza wasiwasi katika nchi zingine duniani, wanasiasa, wachumi na viongozi wengi wanaogopa kuitembelea Iraq, wakati wote vyombo vya habari vinaripoti matukio ya ugaidi na mambo mengine kama vile ujenzi wa taifa na miradi ya kimaendeleo haitangazwi”.

Akabainisha pia: “Hakika Marjaa Dini mkuu ana nafasi muhimu katika kuwafanya watu wajitolee kupambana na magaidi wa Daesh, alifanikiwa kulilinda taifa na shari zao na bado anaendelea kutoa ushauri wa namna ya kutatua matatizo yaliyopo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: