Wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed katika ratiba yao ya hema la nje, wametembelea chuo kikuu cha Ferdusiy nchini Iran

Maoni katika picha
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wametembelea chuo kikuu cha Ferdusiy kilichopo Iran, kupitia ratiba ya hema la Skaut la nje inayo simamiwa na chuo hicho, inayo saidia kuwaboresha kielimu na kivitendo, inasaidia kuboresha viwango vyao vya elimu ya sekula katika hatua mbalimbali za masomo yao ya chuo.

Ugeni huo umepokelewa na kiongozi wa idara ya mahusiano ya kimataifa ya chuo kikuu cha Ferdusiy na jopo la walimu wake, waliwapa mapokezi mazuri, katika kikao chao ilionyeshwa filamu inayo elezea chuo kikuu cha Ferdusiy pamoja na majengo yake na vitivyo iliyo navyo, sambamba na kuelezea selebasi za masomo wanazo tumia na njia za ufundishaji zinazo tumika.

Uongozi wa chuo kikuu cha Ferdusiy uliwatembeza wageni katika majengo ya chuo pamoja na vitengo vyake ikiwemo maktaba kuu, kwa ajili ya kuangalia misingi ya ufundishaji na selebasi za masomo pamoja na vitabu mbalimbali.

Ratiba ya hema la nje haikuishia kutembelea majengo ya chuo kikuu cha Ferdusiy peke yake, bali ugeni huo ulikwenda hadi katika kiwanda cha maziwa ambacho kipo chini ya chuo hicho, kuangalia bidhaa za vyakula vya aina mbalimbali zinazo tengenezwa na kiwanda hicho, kama vile haluwa, juisi, maziwa na zinginezo, zinazo wanufaisha watumishi wa chuo na wanafunzi wao.

Kuhusu ziara waliyo fanya katika kiwanda za maziwa cha chuo kikuu cha Ferdusiy, mkuu wa kitengo cha muongozo wa nafsi na maelekezo ya kimaadili katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Hasanaini Mussawi amesema: “Lengo la kutembelea kiwanda ni kutaka wanafunzi waone namna chuo kikuu cha Ferdusiy kinavyo tengeneza bidhaa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya walimu na wanafunzi wake, sambamba na maabara maalumu ya kiwanda ambayo hutumika kupima malighafi kabla ya kuziingiza katika uzalishaji”.

Akaongeza kua: “Kiwanda hicho kipo katika mji wa Mash-had, nacho ni moja ya sehemu za kufanyia utafiti wanafunzi wa masomo ya juu, ni sehemu ya masomo na utafiti wa kielimu pamoja na kimaabara, jambo hilo linamatokeo chanya (mazuri) kielimu na kiuchumi katika taifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: