Maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza mtazamo wake kuhusu mradi wa kuhifadhi kazi za kielimu zilizo fanywa na wairaq

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu zimeanza kutekeleza mtazamo wake wa kufanya mradi wa (Kuhifadhi kazi za kielimu zilizo fanywa na wairaq), ambapo hatua ya kwanza wanakusudia kutunza tafiti za chuo na kuzihifadhi kielektronik, yamesemwa hayo katika warsha ya kielimu iliyo fanyika kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Mustanswiriyya ambacho kinaafikiana na Atabatu Abbasiyya katika mambo mengi ukiwemo mradi huu.

Warsha ya utambulisho wa mradi imefanywa ndani ya maktaba ya chuo kikuu cha Mustanswiriyya na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wabobezi wa mambo ya maktaba pamoja na kundi kubwa la wanafunzi, mradi umetambulishwa na jopo la wataalamu kutoka maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kwa ukamilifu na malengo yake.

Miongoni mwa yaliyo semwa na kiongozi wa idara ya maktaba ya kielektronik Ustadh Ahmadi Majidi Abdulhussein ni: “Utambulisho wa mradi huu pamoja na malengo yake, hakika kila taifa kwa namna yeyote litakavyo kua, lina changamoto za kimaumbile na zisizokua za kimaumbile, changamoto za kimaumbile kwa mfano kutokea kwa tetemeko au moto.. na zisizokua za kimaumbile kwa mfano vita ambavyo ni matokeo ya vitendo vya wanaadamu, changamoto zote hizo Iraq imezipitia, njia bora ya kuhifadhi turathi za Iraq ni kuzihifadhi kielektronik, huu ndio mtazamo wa Atabatu Abbasiyya tukufu na maktaba kuu ya chuo kikuu cha Mustanswariyya, tunajaribu kuhifadhi turathi zetu kupitia picha, kupitia picha tutaweza kupiga hatua moja kwenda mbele, litakapo tokea tatizo la kimaumbile au lisilokua la kimaumbile likapelekea kuharibika kwa nakala zilizopo mkononi bado tutaendelea kuanazo zilizo hifadhiwa kielektronik, na zitaweza kusaidia vizazi vijavyo”.

Hali kadhalika Shekh Mahmudu Swafi mkuu wa kituo cha Abulfadhil Abbasi (a.s) cha masomo ya takhasusi amesema kua: “Hakika mradi wa kuhifadhi kazi za kielimu zilizo fanywa na wairaq ni muhimu sana, fikra hii ilitolewa mbele ya vyuo vikuu, na chuo kikuu cha Mustanswariyya kikawa cha kwanza kushirikiana na maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inashirikiana na sisi katika mradi huu, imetufungulia maktaba zake zote na kutupa ruhusa ya kupiga picha nakala kale na kuziweka katika muundo wa namba kwa ajili ya wepesi wa kuhifadhika kwake na kupatikana kwake pale zitakapo hitajika, ili kufanikisha kazi hii kuna hatua tatu, ambazo ni:

  • 1- Kuhifadhi sehemu muhimu.
  • 2- Kupewa nafasi ya kutumia barua za chuo zilizo wekwa namba, na kuhakiki uharaka wa kuangalia vitabu (machapicho).
  • 3- Wepesi wa kukopi kwa kutumia namba tofauti na kuzihifadhi sehemu tofauti bila kutumia nafasi kubwa pamoja na kuhifadhi nakala yake ya karatasi.

Atabatu Abbasiyya tukufu ilizungumza mambo hayo katika mlango wa msaada, kusaidiana na kushauriana baina yao, naye Ustadh Aisar Abdul-Amiri amesema kua: “Tunatekeleza mradi muhimu wa kitafa mradi unaolenga kuhifadhi turathi za kielimu za wairaq, waliotumia elimu za wanachuoni kuonyesha njia vizazi vyetu na kuwa mwongozo wa kielimu kwa taifa letu kipenzi, kwa hiyo ni lazima tufanye kazi kubwa ya kutunza turathi hizo kama wao walivyo fanya kazi kubwa ya kuziandaa.

Kwa juhudi za pamoja zinazo fanywa na maktaba mbili, maktaba kuu ya chuo kikuu cha Mustanswariyya na maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya utafiti na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi huu uliopewa jina la (Kuhifadhi kazi za kielimu zilizo fanywa na wairaq) na kuwa mradi pekee hapa Iraq unaotekelezwa kisasa kwa kutumia tafiti na nadhariya ya namba”.

Mwisho wa warsha kulikuwa na nafasi ya maswali na majibu kuhusu mradi huu, wahudhuriaji wakapewa vipeperushi vya kutambulisha mradi, waliusifu mradi huu na kupongeza kazi nzuri iliyo fanywa. Inayo onyesha wazi mafanikio ya mradi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: