Mwezi kumi na tatu Jamadal Thani ni siku yenye machungu makubwa, kwani ndio siku aliyo fariki Ummul Banina (a.s), mama wa Abulfadhil Abbasi (a.s), mama huyu mtukufu alikua na nafasi maalumu katika maisha yake na kiongozi wa waumini (a.s), sio katika majukumu ya nyumbani peke yake, bali alikua na umuhimu kwa watoto wake pia, alikua na subira uaminisu na utiifu, aliimarisha mshikamano na utukufu katika nyumba ya kiongozi wa waumini.
Alikua (a.s) miongoni mwa wanawake watukufu wanaofahamu haki za Ahlulbait (a.s), alikua mfasaha, mwenye zuhudi na mchamungu, baadhi ya wanahistoria wanasema kua mapenzi yake kwa watoto wa Zaharaa (a.s) yalikua makubwa zaidi kushinda mapenzi yake kwa watoto wake wanne –Abbasi na ndugu zake- (a.s), bali yeye ndiye aliwatoa waende kumnusuru Imamu wao na ndugu yao Abu Abdillahi Hussein (a.s), ambapo walijitolea na kuuwawa kishahidi mbele yake katika vita ya Karbala.
Baada ya mauwaji ya Karbala Ummul Banina (a.s) alidumu katika ibada na huzuni ya muda mrefu kutokana na kuwakosa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na tukio la kuumiza zaidi ni kuuwawa kwa watoto wake wanne kwa wakati mmoja wakiwa pamoja na kipenzi cha Mwenyezi Mungu Imamu Hussein (a.s), bila kusahau hayo yametokea baada ya kifo cha mume wake kiongozi wa waumini (a.s), baada ya kifo cha mume wake aliendelea kuwatumikia watoto wake wajukuu wa Mtume (s.a.w.w) Hassan na Hussein (a.s) na mabwana wa vijana wa peponi, na alimtumikia pia Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), bila shaka atapata malipo makubwa, naye ukafika wakati wa kuondoka duniani, akafariki mwezi kumi na tatu Jamadal Thani mwaka wa (64) hijiriyya kama alivyo sema Bairu Jundi katika kitabu cha (Matukio ya siku) na Sayyid Muhammad Baaqir Qurrah Baaghi katika kitabu cha (Kanzul-matwaalibu) na wengineo, katika kitabu cha (Ikhtiyaraat) kutoka kwa A’amash anasema: (Niliingia kwa Imamu Zainul-Aabidina Ali bun Hussein (a.s) katika siku ya mwezi kumi na tatu Jamadal Thani, ilikua siku ya Ijumaa, akaingia Fadhil mtoto wa Abbasi akiwa analia kajaa huzuni, akamwambia: bibi yangu Ummul Banina amefariki).
Amani iwe juu yake mama huyu mwema mtakasifu, mtekelezaji mwenye ikhlasi, aliye mliwaza Zaharaa (a.s) katika msiba wa Hussein (a.s), akamwakilisha katika kufanya maombolezo, hangera kwake na kwa kila atakaye fuata nyayo zake, amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo kufa na siku atakayo fufuliwa kuwa hai kwa idhini ya Mola wake.