Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (16 Jamadal Thani 1440h) sawa na (22 Februari 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) Marjaa Dini mkuu amezungumzia nukta nyingi za kimaadili na kimalezi zinazo gusa jamii yetu ya sasa, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Tukihisi kuwajibika tutatafuta utatuzi.
  • - Tusipo hisi tatizo na kuwajibiba bila shata utatuzi utabaki unasubiri mtatuzi.
  • - Lazima kuwe na mazingira ya jumla ya kutatua tatizo.
  • - Kawaida kila tatizo linautatuzi wake lakini kuna baadhi ya mambo yanahitaji nguvu ya jamii.
  • - Tatizo linapo enea kwa wengi na kudhuru jamii sisi ndio waathirika wakubwa.
  • - Tatizo litaanza kuathiri familia, barabara na soko na linaanza kuvunja jengo muhimu linalo tegemewa na kila mtu.
  • - Baadhi ya matatizo yameanza kuathiri familia na sekta ya elimu.
  • - Mazingira kwa ujumla hayamuachi mkubwa wala mtoto.
  • - Tumeingia katika hali ya vurugu ambayo haiwezi kuisha ispokua kwa kupatikana mtatuzi makini.
  • - Uwelewa na ujuzi unahitaji kuendelezwa.
  • - Sio kila mtu anayesema mimi najua kweli anajua.
  • - Maana ya uwelewa ni kutambua mazingira tunayo ishi.
  • - Uwelewa ni ujuzi unao muwezesha mwanaadamu kujua namna ya kutatua matatizo ya kijamii kabla hayajaleta madhara makubwa.
  • - Baadhi ya wakati kuna tamaduni huwa ni sehemu ya tatizo.
  • - Kuna mambo ambayo ni hatari kwa jamii lazima kila mtu ayazingatie.
  • - Kila mtu anamsukumo wa kufanya au kutofanya jambo.
  • - Wakati fulani msukumo huo hutokana na yeye mwenyewe.
  • - Wakati mwingine msukumo huo huwa wa kidini, kisheria na kitamaduni.
  • - Baadhi ya mambo yanamahala na muda wake.
  • - Tunapo ondoa sehemu na muda katika mambo hayo tunatengeneza vurugu.
  • - Mtu anapokua nyumbani kwake anauhuru ambao hawezi kuupata anapokua barabarani.
  • - Utamaduni usipo lindwa hutokea vurugu.
  • - Mwanaadamu mwenye misingi ya Dini anajua kinachofaa na kisichofaa na hawezi kwenda kinyume na Dini yake.
  • - Kinga ya Dini ndio bora zaidi.
  • - Kuna baadhi ya mambo yasipo pata nguvu ya kisheria na kuacha kila mtu afanye anavyo jisikia inakua vurugu.
  • - Kinga ya kiutamaduni ni pale mtu atakapo weza kusema jambo hili ni aibu sio utamaduni wetu.
  • - Mtu anapo acha Dini na akavunja sheria na kupuuza utamaduni itatokea fujo na vurugu.
  • - Sheria ikitoweka vurugu hutawala.
  • - Kila jamii lazima iwe na kitu kinacho zuwia isiangamizwe.
  • - Lazima tushikamane na tujenge jamii yenye mshikamano.
  • - Hakuna utatuzi ispokua ni kurudi katika misingi ya Dini, sheria na utamaduni kwa namna ambayo havitagongana.
  • - Tukijitenga na misingi yote matokeo hayatasubiri baadae yataonekana wazi sasa hivi.
  • - Hali ya jamii inataka kila mtu awajibike.
  • - Kila mtu awajibike kwa ukamilifu katika kulinda jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: