Mmoja wa mahafidhi wa Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani apata nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani ya kitaifa kwa wasio ona…

Maoni katika picha
Haafidhu wa Qur’ani bwana Muhammad Abdu-Ali Kumashi ambaye ni mmoja wa maustadhi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la Hindiyya, amepata nafasi ya kwanza katika mashindano ya pili ya kuhifadhi Qur’ani ya kitaifa kwa wasio ona, ikiwa kama sehemu ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa, mashindano haya yameandaliwa na kituo cha kitaifa cha maarifa ya Qur’ani chini ya uongozi wa wakfu Shia, kikao chake cha kufunga mashindano kimefanyika katika mji wa Najafu Ashrafu kwa kushirikiana na uongozi wa mazaru wa swahaba mtukufu Maitham Tammaar (r.a).

Washiriki wa mashindano haya walikua (22) kutoka mikoa yote ya Iraq, ni wale walioshinda katika mashindano ya awali yaliyo andaliwa na kituo cha kitaifa katika mji wa Bagdad na kwenye mikoa mingine, kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kuingia katika mashindano ya kimataifa, yamesimamiwa na kamati ya majaji wa kimataifa walio bobea katika maswala ya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: