Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi wa stara na hijabu: Idara ya wahadhiri wa kike inafanya mahafali ya kutoa zawadi kwa wanafunzi walio fika umri wa kuwajibikiwa na sheria (kubalekhe)…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi wa stara na hijabu Fatuma Zaharaa (a.s), idara ya wahadhiri wa kike inafanya mahafali ya kuwapa zawadi wanafunzi wa kike katika mkoa wa Karbala waliofika umri wa kuwajibikiwa na sheria (kubalekhe).

Katika kuangazia jambo hili ambalo ni moja ya harakati zinazo fanywa na idara ya wahadhiri wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeongea na makamo kiongozi mkuu wa idara ya wahadhiri wa kike Ustadhat Taghridi Abdul-khaliq Tamimi ambaye amesema kua: “Hakika umri wa kuwajibikiwa na sheria ni umri wenye mabadiliko makubwa kwa msichana, mahafali hii inayo shirikisha wanafunzi kutoka shule za Karbala inalenga kuwaandaa wanasichana na kipindi hiki cha kihistoria katika uhai wa msichana, kipindi cha kuingia katika umri wa kuwajibikiwa na sheria, kinacho jenga uhusiano wa msichana na Mola wake kwa kusimamisha swala na namna atakavyo ishi na jamii kwa kushikamana na hijabu”.

Akaendelea kusema: “Huu ndio wakati wa kutekeleza maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo: (Sikuwaumba majini na binaadamu ispokua kwa ajili ya kuniabudu) mwanamke anapo sitirika nusu ya jamii husitirika, bali mwanamke ndio msingi wa jamii yeye ndie ambaye hujenga familia yenye mshikamano na yenye kufuata misingi ya kiislamu, msichana ndiye mlengwa wa fikra potofu zinazo sambazwa katika zama zetu kupitia vyombo vinavyo tumika kuvunja maadili ya wasichana na kuwavua heshima yao pamoja na kuwaweka mbali na Mwenyezi Mungu mtukufu kisha kuwaweka mbali na jamii, katika mahafali hii imeandaliwa ratiba inayo endana na uwezo wa akili zao na kuna wahadhiri mahiri wanaozungumza mambo ya sasa na ya baadae”.

Akasema: “Ratiba tuliyo andaa inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Mhadhara kuhusu hijabu na umuhimu wake kwa wasichana.
  • - Usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na tafsiri ya baadhi ya aya zinazo zungumzia hijabu.
  • - Masomo kuhusu historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuangazia hadithi zao pamoja na kuzilinganisha na mazingira halishi tunayo ishi.
  • - Masomo ya fiqihi na aqida yanayo endana na umri wao.
  • - Vipindi mbalimbali vya viburudisho.

Katika mahafali hiyo wanafunzi wakapewa nguo za kuswalia, pamoja na zawadi za kutabaruku na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kua umri wa kuwajibikiwa na sheria umeelezewa na Dini tukufu ya kiislamu na Atabatu Abbasiyya inayapa umuhimu mafundisho hayo, kwa ajili ya kujenga msingi imara na uwelewa, umri huu ni kipindi muhimu sana kielimu katika kumtoa mwanafunzi kwenye mstari wa hatari na kumuweka katika mstari wa sawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: